Nikola Tavelic
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nikola Tavelić (Šibenik, Korasya, 1340 hivi - Yerusalemu, leo kati ya Israeli na Palestina, 14 Novemba 1391) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo, padri na mmisionari katika Nchi takatifu ya Yesu.


Pamoja na wenzake Deodato wa Ruticinium, Stefano wa Cuneo na Petro wa Narbone, alichomwa moto kwa kuwa walihubiri hadharani kwa ushujaa dini ya Kikristo mbele ya Waislamu, wakimkiri kwa uimara Kristo Mwana wa Mungu [1].
Pamoja nao alitangazwa na Papa Leo XIII kuwa mwenye heri mwaka 1889, halafu na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu mfiadini tarehe 21 Juni 1970. Ni wa kwanza kutoka Kroatia.
Sikukuu yao ni tarehe waliyouawa na Waislamu waliowahubiria Injili[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads