Papa Boniface II
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Boniface II alikuwa Papa kuanzia tarehe 20/22 Septemba 530 hadi kifo chake tarehe 17 Oktoba 532[1][2]. Alitokea Roma, Italia[3], lakini alikuwa Mwostrogoti, Papa wa kwanza mwenye asili ya Kigermanik[4].

Alimfuata Papa Felisi IV akafuatwa na Papa Yohane II.
Aliteuliwa na mtangulizi wake awawekwa wakfu na kuvishwa taji la kipapa tarehe 22 Septemba 530. Mpinzani wake, antipapa Dioscorus, aliyechaguliwa na wingi wa mapadri wa Roma, aliwekwa wakfu siku hiyohiyo lakini alifariki siku 22 baadaye.
Uamuzi muhimu zaidi aliouchukua ni kupitisha mafundisho ya Mtaguso wa Orange (529) kuhusu haja ya neema kwa wokovu[5].
Remove ads
Tazama pia
Maandishi yake
- Documenta Catholica Omnia (Kilatini)
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads