Papa Hilarius

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Hilarius
Remove ads

Papa Hilarius alikuwa Papa kuanzia tarehe 19 Novemba 461 hadi kifo chake tarehe 29 Februari 468[1]. Alitokea Sardinia, Italia[2].

Thumb
Papa Hilarius.

Alimfuata Papa Leo I akafuatwa na Papa Simplicio.

Chini ya Papa Leo I alikuwa shemasi mkuu na alipigania haki za Kanisa. Pia alitumwa naye kama balozi kwenye Mtaguso wa pili wa Efeso (449) alipopata matatizo makubwa [3] kwa kumtetea Flaviano wa Kostantinopoli[4].

Baada ya kuchaguliwa aliendeleza sera za Papa Leo I kuhusu mamlaka ya Kanisa la Roma [5] na alipambana na makundi yaliyofarakana naye[3].

Aliandika barua muhimu kuhusu imani Katoliki ili kuthibitisha mitaguso mikuu ya Nisea, Efeso na Kalsedonia akiimarisha pia mamlaka ya Papa wa Roma kwa kuonyesha nafasi yake ya kwanza katika Kanisa lote [6].

Hatimaye anasifiwa kwa ujenzi wa makanisa mbalimbali mjini Roma.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 29 Februari (28 Februari katika miaka mifupi)[7], lakini pia 17 Novemba.

Remove ads

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads