Papa Leo IX

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Leo IX
Remove ads

Papa Leo IX (21 Juni 100219 Aprili 1054) alikuwa Papa kuanzia tarehe 2 au 12 Februari 1049 hadi kifo chake[1]. Alitokea Alsace, leo nchini Ufaransa[2].

Thumb
Mt. Leo IX.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Bruno wa Eguisheim-Dagsburg[3].

Alimfuata Papa Damaso II akafuatwa na Papa Viktor II.

Akielekea Roma kwa ajili ya kutawazwa, alikutana na abati Hugo wa Cluny na kumchukua mmonaki Hildebrando ambaye akaja kuwa Papa Gregori VII[4].

Alikuwa Papa bora kutoka Ujerumani katika Karne za Kati, akijitahidi kupambana na maovu ya wakati ule[5][6], ingawa kutokana na utawala wake lilitokea farakano na Kanisa la Kigiriki (Farakano la mwaka 1054)[7] .

Alitangazwa na Papa Gregori VII kuwa mtakatifu mwaka 1082.

Sikukuu yake huadhimishwa kwenye tarehe ya kifo chake[8].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Vyanzo

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads