Papa Pius I

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Pius I
Remove ads

Papa Pius I alikuwa papa kuanzia takriban 142/146 hadi kifo chake takriban 157/161[1]. Alitokea Aquileia, Italia[2][3] na labda baba yake aliitwa "Rufinus".[4]. Hakika alikuwa ndugu wa Herma, aliyewahi kuwa mtumwa akawa mwandishi wa kitabu maarufu "Mchungaji"[5].

Thumb
Papa Pius I.

Alimfuata Papa Hyginus akafuatwa na Papa Anicetus.

Alipinga uzushi wa Gnosi hata kumtenga Marcio na Kanisa[6][7].

Chini yake, Yustino alifundisha katekesi mjini Roma na kupambana na aina mbalimbali za Gnosi [8].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu[9].

Sikukuu yake ni tarehe 11 Julai[10].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads