Papa Viktor I

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Viktor I
Remove ads

Papa Viktor I (au Victus I) alikuwa Papa kuanzia takriban 186/189 hadi kifodini chake takriban 197/201[1].

Thumb
Papa Vikta I katika dirisha la kioo cha rangi (Semmering, Austria).

Alimfuata Papa Eleutero akafuatwa na Papa Zefirini.

Alikuwa Papa wa kwanza kutokea Afrika, labda Leptis Magna, leo nchini Libya.

Anajulikana hasa kwa msimamo wake mkali kuhusu suala la tarehe ya Pasaka, wakati kabla ya yeye kufanywa Papa, tofauti kuhusu tarehe hiyo haikusababisha farakano.[2] Kwa kuwa alitenga na Kanisa walioadhimisha Pasaka ya Kikristo siku moja kabla ya Pasaka ya Kiyahudi, si Jumapili iliyoifuata kama huko Roma[3], Ireneo na wengineo walimlaumu, kadiri alivyoandika Eusebi wa Kaisarea.

Hata hivyo, tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 28 Julai[4].

Remove ads

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads