Ruvu (Pwani)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Ruvu (maana)
Ruvu (zamani Kingani pia[1]) ni mto wa Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Pwani nchini Tanzania.
Unapokea hasa maji ya upande wa mashariki wa milima ya Uluguru na kuyapeleka Bahari Hindi.
Ruvu hii haina uhusiano na mto Jipe Ruvu wa mkoa wa Kilimanjaro / Upare.
Remove ads
Beseni la mto
Beseni la mto lina eneo la takriban kilomita za mraba 17,700 [2]
Ndani yake kuna maeneo matatu ya utiririshaji yaani, Ruvu ya Juu, Ngerengere na Ruvu ya Chini. Ruvu ya Juu inapokea maji kutoka mtelemko wa mashariki wa Uluguru, Ngerengere kutoka mtelemko wa magharibi na Ruvu ya chini kutoka milima mingine.
Tabianchi ya beseni inabadilika kati ya mahali na mahali; milima ya juu hupokea mvua zaidi kuliko tambarare za chini. Mwezi unaoleta mvua nyingi ni Aprili.
Remove ads
Chanzo cha maji ya Dar es Salaam
Ruvu ya Pwani ni chanzo kikuu cha maji kwa jiji la Dar es Salaam. Hili ni tatizo kwa sababu kiasi cha maji yake huzidi kupungua kutokana na uharibifu wa misitu na mabadiliko ya tabia ya nchi.[3]
Tangu mwaka 1958 kiasi cha maji ya Ruvu kinapimwa kwenye daraja la barabara kuu A7 takriban kilomita 40 kabla ya mdomo wake. Kwa wastani zimepita hapa m³ 61 kwa sekunde. Kiwango hiki kinabadilika sana kulingana na majira ya mvua na ya ukame.
Kiwango cha maji (mita za ujazo kwa sekunde) kinachopita kwenye daraja la Ruvuma karibu na Mlandizi kwa mwezi
(Ilikadiriwa kwa kutumia data za kipindi cha miaka 46 1958–2004)[4]

Serikali inapanga kujenga lambo na kuanzisha bwawa la Kidunda kwenye njia ya mto Ruvu takriban kilomita 70 upande wa kusini wa Chalinze. Bwawa hili linakusudiwa kudhibiti mwendo wa maji kwenye mto Ruvu na kuongeza maji kwa ajili ya vituo vya kuchukua maji ya Dar es Salaam (DAWASA) wakati wa ukame. [5][6]
Remove ads
Tazama pia
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads