Ubatizo wa Bwana

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ubatizo wa Bwana
Remove ads

Ubatizo wa Bwana ni sikukuu ya liturujia inayoadhimisha fumbo la Yesu kubatizwa na Yohane Mbatizaji katika mto Yordani kabla hajaanza utume wake mwenyewe.

Thumb
Ubatizo wa Kristo ulivyochorwa ukutani na Giotto mwaka 1305 hivi (Cappella Scrovegni, Padua, Italia).

Ndiyo sababu inatimiza kipindi cha Noeli kinachoadhimisha kwa muda mfupi miaka yote ya maisha yaliyofichika ya Yesu, mingi ikiwa aliitumia kama seremala kijijini Nazareti.

Kwa kuwa Yesu aliacha maisha hayo akaanza utume wake miezi tu baada ya Yohane Mbatizaji, jamaa yake, kuwatikisa Wayahudi wote akihubiri wawe tayari kwa ujio wa mtu mkubwa zaidi, akisema, “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto” (Math 3:11).

Remove ads

Marejeo ya Kiswahili

  • Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 11-12

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ubatizo wa Bwana kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads