Ulama

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ulama
Remove ads

Ulama (pia: Ulema, kutoka Kiarabu علماء ʿulamāʾ) ni namna ya kutaja wataalamu wa dini katika Uislamu.

Ukweli wa haraka
Remove ads

Mamlaka na uwezo wao ni tofauti katika jamii za Kiislamu kufuatana na mapokeo tofauti. Katika madhehebu ya Shia wana athira kubwa zaidi.

Kati ya Waislamu ulema huulizwa kuhusu uelewano wa sharia na vipengele vingine vya imani.

Neno "ulama" latokana katika lugha ya Kiarabu na hapa ni wingi wa aalim (ar. عالِم) inayomaanisha "mtu mwenye elimu, mtaalamu". Neno hili linaweza kutaja wataalamu wa kila fani lakini inamaanisha hasa wataalamu wa dini[1].

Remove ads

Matawi ya elimu

Kimapokeo ulema hujifunza Quran, tafsir (namna ya kuelewa Qurani), Sunnah na ahadith, shariah (kanuni za imani), fiqh (namna ya kutumia sharia) na kalam (theolojia au mafundisho kuhusu imani).

Marejeo

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads