Utamaduni wa Zimbabwe

From Wikipedia, the free encyclopedia

Utamaduni wa Zimbabwe
Remove ads

Utamaduni wa Zimbabwe unajumuisha mchanganyiko wa makabila mbalimbali yenye mila na desturi za kipekee.

Ukweli wa haraka Idadi ya makabila, Lugha rasmi ...
Thumb
Ngoma za kitamaduni nchini Zimbabwe

Washona na Wandebele ndio makabila makubwa zaidi nchini humo, ikiwa takwimu zinaonesha Washona ndio kabila mama lenye makadirio ya zaidi ya asilimia 80 za wakazi na kufuatiwa na Wandebele lenye makadirio ya asilimia 14 ya wakazi, huku makundi mengine ya kitamaduni kama Watonga, Wachewa, Wavenda na mengine mengi huongeza utofauti na utajiri wa utamaduni wa nchi ya Zimbabwe.[1]

Remove ads

Historia

Ustaarabu wa kale wa Zimbabwe Kuu, uliodumu kati ya karne ya 11 na 15, unahesabiwa kuwa nguzo muhimu ya historia ya kitamaduni nchini humo. Mji huo wa mawe uliokuwa kituo cha biashara ya dhahabu na pembe za ndovu ulikuwa na ushawishi mkubwa katika eneo lote la Kusini mwa Afrika. Baada ya kuporomoka kwake, dola zingine kama Mutapa na Rozvi ziliibuka na kuendeleza urithi huo wa kifalme na kijamii.

Mnamo karne ya 19, kundi la Wazulu waliounda dola ya Ndebele walihamia eneo la kusini mwa Zimbabwe ya leo, na hivyo kuongeza utofauti wa kijamii na kitamaduni. Kipindi cha ukoloni (1890–1980) kilileta mabadiliko makubwa ya kijamii, lakini pia kilichangia katika kuhamasisha harakati za uhuru na utambulisho wa kitaifa ulioshikilia baadhi ya mila za jadi.[1]

Remove ads

Lugha

Lugha nyingi zinazungumzwa, au kihistoria zimezungumzwa, nchini Zimbabwe. Tangu kupitishwa kwa katiba mpya 2013, Zimbabwe ina lugha rasmi 16[2], ambapo ni pamoja na Chewa, Chibarwe, Kiingereza, Kalanga, Koisan, Nambya, Ndau, Ndebele, Shangani, Shona, Sotho, Tonga, Tswana, Venda, Xhosa na Lugha ya alama. Imekua ni mojawapo ya nchi chache barani Afrika zilizo na lugha rasmi nyingi, na hii ni ishara ya utofauti mkubwa wa kitamaduni. Utamaduni huu umeendelea kupitia muziki, ngoma, sanaa, mavazi, chakula cha jadi, na imani za kijadi ambazo bado zinaheshimiwa hadi leo.

Idadi kubwa ya watu huzungumza lugha za Kibantu, kama vile Kishona na Kindebele. Kiingereza huzungumzwa sana mijini, lakini katika maeneo ya vijijini huzungumzwa lugha asilia. Elimu nchini Zimbabwe inafundishwa kwa Kiingereza, Kishona na Kindebele. Shule nyingi za msingi za vijijini hufundishwa kwa lugha ya asili hadi darasa la tatu, baada ya hapo huanza kufundishwa kwa Kiingereza.

Remove ads

Chakula

Thumb
Sadza na rosti ya nyama ya mbuzi na mboga za majani

Kama ilivyo katika nchi zingine za kiafrika Zimbabwe inategemea chakula kinachotokana na kilimo cha mazao kama mahindi, mtama, na kunde. Chakula kikuu ni Sadza, ambapo ni uji mzito wa unga wa mahindi na huliwa pamoja na mboga za majani (muriwo), nyama kama ya ng’ombe, kuku au samaki. Katika baadhi ya maeneo, samaki wadogo waliokaushwa kama kapenta, na mboga kama derere hupikwa kama viambatanisho.

Vitafunwa vya asili ni pamoja na maputi (mahindi ya kuchoma), wakati vinywaji maarufu ni pamoja na maheu, kinywaji kilichotengenezwa kwa kuchachua unga wa mahindi.

Viungo vya nje

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads