Veronika Giuliani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Veronika Giuliani (Mercatello sul Metauro, Marche, Italia, 27 Desemba 1660 - Città di Castello, Umbria, Italia, 9 Julai 1727) alikuwa mmonaki wa urekebisho wa Wakapuchini wa Utawa wa Mt. Klara.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira. Ingawa aliheshimiwa hivyo mara baada ya kufa, kesi ya kumtangaza rasmi ilicheleweshwa na uchunguzi wa maandishi yake marefu.
Papa Pius VII ndiye aliyemtangaza mwenye heri mnamo Juni 1804, halafu Papa Gregori XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 26 Mei 1839.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyofariki dunia[1] au kesho yake.
Remove ads
Maisha
Maandishi yake mwenyewe yanasimulia alivyoanza kujaliwa karama za pekee akiwa na umri wa miaka 3 tu, alipokuwa anaitwa Orsola.
Alijiunga na Waklara Wakapuchini wa monasteri ya Città di Castello mwaka 1667 ambapo akawa abesi tangu mwaka 1716 hadi kifo chake.
Kwa namna ya pekee aliambatana kiroho na kimwili na Yesu msulubiwa kadiri ya karama ya Fransisko wa Asizi.
Kwa ajili hiyo alifungwa siku 50 ili kuchunguzwa kwa makini, akivumilia jaribu hilo kwa utiifu na subira vya ajabu[2]
Hatimaye Kanisa Katoliki limekubali ukweli wa madonda matakatifu aliyosema kuwa nayo tangu tarehe 5 Aprili 1697 hadi kifo chake.
Remove ads
Maandishi
Kwa agizo la padri aliyemuongoza kiroho, aliandika kirefu (kurasa 22,000 kwa mikono bila ya sahihisho lolote) kumbukumbu za maisha yake yote, ambazo zilitolewa baada ya kifo chake kwa jina Il Tesoro Nascosto (ni magombo 36).
Kutokana na shajara hiyo, Veronika Giuliani anahesabiwa kati ya Wakristo wanasala waliojaliwa mang'amuzi ya juu zaidi.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads