Wandrili
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wandrili (pia: Wandregisel; Verdun, 605 - 22 Julai 668) alikuwa afisa katika ikulu ya mfalme Dagoberti I hadi mwaka 629 alipojifanya mmonaki chini ya Balderiki kisha kukubaliana na mke wake.
Baadaye akaishi upwekeni akaanza kufuata kanuni ya Mt. Kolumbani. Mwisho alipewa upadrisho na askofu Dado akaanzisha msituni monasteri ya aina hiyo, akaiongoza kama abati hadi kifo chake[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Vyanzo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads