Warekoleti

From Wikipedia, the free encyclopedia

Warekoleti
Remove ads

Rekoleti (kutoka Kilatini: Recollecti (yaani Waliojikusanya kutafakari [1]) walikuwa watawa wa mashirika mbalimbali, hasa Wafransisko na Waaugustino, waliolenga urekebisho wa maisha ya pamoja kuanzia karne ya 16.

Tawi la Wafransisko liliungana na Ndugu Wadogo wengine mwaka 1897, lakini lile la Waagustino linaendelea hadi leo likiwa na wanashirika karibu elfu moja.

Thumb
Dirisha la kioo cha rangi likimuonyesha Mt. Yohane Wall akiadhimisha Misa kwa siri katika chumba cha ukumbi wa Harvington.
Remove ads

Historia ya Ndugu Wadogo Warekoleti

Huko Italia, ndugu waliojikusanya katika makao ya upwekeni kuanzia mwaka 1535 (mkutano mkuu ulipowaruhusu ili kuzuia wengine wengi wasiwakimbilie Wakapuchini), kisha kuongezeka waliwekwa moja kwa moja chini ya Mtumishi mkuu tu (1579), wakapewa katiba maalumu (1595), ruhusa za pekee sana (1596), hatimaye Kiongozi mkuu na mkutano mkuu wa kwao. Hivyo mamlaka ya Mtumishi wa OFM kwao ikawa jina tu. Hao waliitwa Wareformati.

Kumbe Ufaransa makao ya upwekeni hayakustawi sana hadi mwisho wa karne XVI. Mwaka 1575 yalikuwa na watawa 50 tu. Lakini mwaka 1601 walioishi huko walipewa na Kanisa Mkurugenzi mwenye mamlaka pana sana; hapo wakaenea haraka kwa msaada wa mfalme Henri IV wa Ufaransa na wa Papa KlementI VIII, hata kanda zote za Ndugu Wadogo wa Ujerumani na Uholanzi zikajirekebisha na kujiunga nao, wakaitwa Warekoleti. Mmojawao ni John Wall (+1679), aliyefia dini huko kwao Uingereza.

Mwaka 1700 walikuwa 9,200 na mwaka 1762 hivi walikuwa 11,000 katika konventi 490 za kanda zao 22[2]. Baadhi yake zilikuwa nje ya Ulaya, katika nchi mbalimbali za Amerika ya Kilatini, na huko Kanada, Ufilipino na Malaka[3].

Baada ya dhuluma za serikali za Zama za Mwangaza na za Mapinduzi ya Kifaransa zilizowapunguza sana, waliobaki walikubali agizo la Papa Leo XIII la kuungana na matawi mengine ya Ndugu Wadogo, wakiweka tu sharti la kwamba ufukara ufuatwe kwa uangalifu.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads