Halmashauri ya Kiekumeni ya Makanisa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Halmashauri ya Kiekumeni ya Makanisa (kwa Kiingereza: World Council of Churches, kifupi WCC) ni muundo wa kimataifa unaokusudiwa kuunganisha madhehebu ya Ukristo. Ilianzishwa mwaka 1948.
Makao makuu yako Geneva, Switzerland.[1]
Halmashauri hiyo ni tunda la juhudi za ekumeni na kauli yake ya msingi ni kwamba: "Halmashauri ya Kiekumeni ya Makanisa ni jumuia ya makanisa yanayomkiri Bwana Yesu Kristo kuwa Mungu na Mwokozi kadiri ya Maandiko, na kwa sababu hiyo yanajitahidi kutekeleza pamoja wito unaoyaunganisha yote kwa utukufu wa Mungu pekee: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu".[2]
Kati ya wanachama 356 kuna Makanisa mengi ya Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Wakatoliki wa Kale, Ushirika wa Kianglikana, Waprotestanti kama vile Walutheri, Wamenno, Wamethodisti, Wamoravian na Wapresbiteri, Wabaptisti na baadhi ya Wapentekoste.[3] Kumbe Kanisa Katoliki si mwanachama, ingawa linatuma wawakilishi wake katika mikutano.[4]
Kwa jumla yanawakilisha Wakristo zaidi ya milioni 600 katika nchi 110 na jumuia 520,000 zinazohudumiwa na mapadri na wachungaji 493,000.[5]520,000 local congregations served by 493,000 pastors and priests, in addition to elders, teachers, members of parish councils and others.[6]
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
