Bad

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bad
Remove ads

Bad ni jina la kutaja albamu ya saba ya mwanamuziki, mtayarishaji wa rekodi, mwimbaji, mfanyabiashara, kabaila, na mhisani wa Kimarekani, Michael Jackson. Albamu ilitolewa mnamo tar. 31 Agosti 1987 na studio ya Epic/CBS Records. Rekodi ya albamu hii ilitolewa karibuni miaka mitano tangu kutoka kwa albamu ya awali. Miaka ishirini baada ya kutolewa, albamu imeuza takriban nakala zaidi ya milioni 30 kwa dunia nzima, na kopi milioni 8 ziliuzwa nchi za nje kwa kupitia Marekani peke yake. Bad ni albamu ya kwanza, na ndiyo hadi sasa albamu pekee, iliyoweza kuingiza single tano katika Billboard Hot 100 zikiwa nafasi ya 1.[3]

Ukweli wa haraka Studio album ya Michael Jackson, Imetolewa ...

Katika albamu hii, Jackson ameonekana kuwa huru zaidi kupita zile albamu zake za mbili za awali, Off the Wall na albamu yenye mauzo bora kwa muda wote, Thriller. Humu katunga nyimbo tisa katika kumi na moja za albamu, na amesaidia kutunga na kutayarisha wimbo wa "Man in the Mirror". Pia humu amekuja na sura mpya ya mshangao.

Albamu iliendelea kupata mafanikio makubwa katika miaka ya 1980 na imeshinda tuzo mbili za Grammy, moja kwa Muziki Bora wa Video - Leave Me Alone na nyingine kwa ajili ya Uhandisi Bora wa Albamu, Bruce Swedien na Humberto Gatica.[4] Mnamo mwaka 2009, Bad pia, imewekwa nafasi ya 43 katika orodha ya Albamu Bora 100 za Karne za MTV zilizoorodheshwa na VH1.[5] Albamu pia iliwekwa nafasi ya 202 katika orodha ya gazeti ya Rolling Stone, Albamu Bora ya Karne.[6]

Remove ads

Historia

Orodha ya nyimbo

Maelezo zaidi #, Jina ...
Maelezo zaidi Toleo la CD la 1988, # ...
Maelezo zaidi "Toleo Maalumu" la 2001, # ...

Toleo la pili la Bad limekuwa na utofauti fulani ukifananisha na lile toleo la mwaka wa 1987:[8]

  • "Bad" inabadiliko ya utayarishaji.
  • "The Way You Make Me Feel" ina utajiri wa sauti za nyuma kuliko ya awali.
  • "I Just Can't Stop Loving You" imeondosha maneno ya mwanzo ya Jackson.
  • "Dirty Diana" imeongezeka kidogo.
  • "Smooth Criminal" imeondosha pumzi za kigiizaji na intro.
Remove ads

Single zake

  1. Julai 1987 - "I Just Can't Stop Loving You" U.S. #1 / UK #1
  2. Septemba 1987 - "Bad" U.S. #1 / UK #3
  3. Novemba 1987 - "The Way You Make Me Feel" U.S. #1 / UK #3
  4. Januari 1988 - "Man in the Mirror" U.S. #1 / UK #21
  5. Aprili 1988 - "Dirty Diana" U.S. #1 / UK #4
  6. Julai 1988 - "Another Part of Me" U.S. #11 / UK #15
  7. Septemba 1988 - "Smooth Criminal" U.S. #7 / UK #8
  8. Januari 1989 - "Leave Me Alone" UK #2
  9. Juni 1989 - "Liberian Girl" UK #13[9]

Chati zake

Maelezo zaidi Chati (1987), Nafasi iliyoshika ...

Matunukio

Maelezo zaidi Nchi, Matunikio ...

Mauzo ya Marekani

Maelezo zaidi Kipindi, Tuzo ya RIAA ...
Remove ads

Marejeo

Maelezo

Tazama

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads