Fransisko Massabki

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Fransisko Massabki (aliuawa Damasko, Syria, 10 Julai 1860) alikuwa Mkristo wa Kanisa la Wamaroni aliyeuawa na Wadruzi kwa sababu alikataa kusilimu[1].

Pamoja naye waliuawa Wafransisko 8: mapadri 6 (Manuel Ruiz, Karmelo Bolta, Engelbati Kolland, Nikanori Ascanio, Petro Nolasko Soler, Nikola Maria Alberca) na mabradha 2 (Fransisko Pinazo na Yohane Yakobo Fernandez) na ndugu zake Abdel Mooti na Rafaeli.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini tangu tarehe 20 Oktoba 2024, alipotangazwa na Papa Fransisko. Kabla ya hapo alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI tarehe 10 Oktoba 1926.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads