Fransisko Pinazo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Fransisko Pinazo

Fransisko Pinazo, O.F.M. (El Chopo, Hispania, 26 Agosti 1802 - Damasko, Syria, 10 Julai 1860) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Waoservanti aliyeuawa na Wadruzi kwa sababu alikataa kusilimu[1].

Thumb
Mchoro rasmi wa wafiadini 11 wa Damasko.

Pamoja naye waliuawa Wafransisko wenzake 7: mapadri 6 (Manuel Ruiz, Karmelo Bolta, Engelbati Kolland, Nikanori Ascanio, Petro Nolasko Soler, Nikola Maria Alberca) na bradha 1 (Yohane Yakobo Fernandez) na ndugu 3 wa Kanisa la Wamaroni (Fransisko, Abdel Mooti na Rafaeli).

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini tangu tarehe 20 Oktoba 2024, alipotangazwa na Papa Fransisko. Kabla ya hapo alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI tarehe 10 Oktoba 1926.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[2].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.