Nikola Maria Alberca

From Wikipedia, the free encyclopedia

Nikola Maria Alberca
Remove ads
Remove ads

Nikola Maria Alberca, O.F.M. (Aguilar de la Frontera, Hispania, 10 Septemba 1830 - Damasko, Syria, 10 Julai 1860) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Waoservanti na padri wa Kanisa Katoliki aliyeuawa na Wadruzi kwa sababu alikataa kusilimu[1].

Thumb
Mchoro rasmi wa wafiadini 11 wa Damasko.

Pamoja naye waliuawa Wafransisko wenzake 7: mapadri 5 (Manuel Ruiz, Karmelo Bolta, Engelbati Kolland, Nikanori Ascanio, Petro Nolasko Soler) na mabradha 2 (Fransisko Pinazo na Yohane Yakobo Fernandez) na ndugu 3 wa Kanisa la Wamaroni (Fransisko, Abdel Mooti na Rafaeli).

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini tangu tarehe 20 Oktoba 2024, alipotangazwa na Papa Fransisko. Kabla ya hapo alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI tarehe 10 Oktoba 1926.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading content...

Marejeo

Viungo vya nje

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads