Engelbati Kolland

From Wikipedia, the free encyclopedia

Engelbati Kolland
Remove ads

Engelbati Kolland, O.F.M. (Ramsau, Austria, 21 Septemba 1827 - Damasko, Syria, 10 Julai 1860) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Waoservanti na padri wa Kanisa Katoliki aliyeuawa na Wadruzi kwa sababu alikataa kusilimu[1].

Thumb
Mchoro rasmi wa wafiadini 11 wa Damasko.

Pamoja naye waliuawa Wafransisko wenzake 7: mapadri 5 (Manuel Ruiz, Karmelo Bolta, Nikanori Ascanio, Petro Nolasko Soler, Nikola Maria Alberca) na mabradha 2 (Fransisko Pinazo na Yohane Yakobo Fernandez) na ndugu 3 wa Kanisa la Wamaroni (Fransisko, Abdel Mooti na Rafaeli).

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini tangu tarehe 20 Oktoba 2024, alipotangazwa na Papa Fransisko. Kabla ya hapo alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI tarehe 10 Oktoba 1926.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads