Manuel Ruiz

From Wikipedia, the free encyclopedia

Manuel Ruiz

Manuel Ruiz, O.F.M. (San Martin de Las Ollas, Hispania, 5 Mei 1804 - Damasko, Syria, 10 Julai 1860) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Waoservanti na padri wa Kanisa Katoliki aliyeuawa na Wadruzi kwa sababu alikataa kusilimu[1].

Thumb
Mchoro rasmi wa wafiadini 11 wa Damasko.

Pamoja naye waliuawa Wafransisko wenzake 7: mapadri 5 (Karmelo Bolta, Engelbati Kolland, Nikanori Ascanio, Petro Nolasko Soler, Nikola Maria Alberca) na mabradha 2 (Fransisko Pinazo na Yohane Yakobo Fernandez) na ndugu 3 wa Kanisa la Wamaroni (Fransisko, Abdel Mooti na Rafaeli).

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini tangu tarehe 20 Oktoba 2024, alipotangazwa na Papa Fransisko. Kabla ya hapo alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI tarehe 10 Oktoba 1926.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[2].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.