Fransisko Saveri
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Fransisko Saveri (jina asili: Francisco de Jasso y Azpilicueta; Javier, Navarra, leo nchini Hispania, 7 Aprili 1506 - kisiwa cha Shangchuan, China, 3 Desemba 1552) alikuwa padri wa Shirika la Yesu, ambalo alichangia kulianzisha pamoja na Ignas wa Loyola.





Baadaye, akisukumwa na hamu yenye ari ya kueneza Injili, alimtangaza Kristo kwa bidii katika nchi nyingi za Ulaya, Afrika na Asia hata akawa kati ya wamisionari maarufu zaidi ya historia ya Kanisa.
Baada ya kuwahubiria makabila mengi ya India, visiwa vya Maluku na vinginevyo, huko Japani aliongoa watu wengi kwenye imani ya Ukristo akafa hatimaye karibu na China bara, ameishiwa nguvu na maradhi na kazi nyingi[1].
Alitangazwa na Papa Paulo V kuwa mwenye heri tarehe 25 Oktoba 1619, halafu Papa Gregori XV akamtangaza mtakatifu tarehe 12 Machi 1622.
Anaheshimiwa na Waanglikana na Walutheri pia.
Remove ads
Sala yake
Ee Mungu wa mataifa yote ya dunia, uukumbuke umati wa Wapagani ambao, ingawa waliumbwa kwa sura yako, hawajakufahamu wewe wala kifo cha Mwanao Yesu Kristo, mwokozi wao.
Fanya kwamba, kwa sala na kazi za Kanisa lako takatifu, wakombolewe kutoka ushirikina wote na utovu wa imani wakaletwe kwenye ibada zako.
Kwa njia ya yule uliyemtuma awe ufufuo na uzima wa watu wote, huyo Mwanao Yesu Kristo, Bwana wetu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads