Fransisko wa Paola

From Wikipedia, the free encyclopedia

Fransisko wa Paola
Remove ads

Fransisko wa Paola (kwa Kiitalia Francesco da Paola; 27 Machi 14162 Aprili 1507) alikuwa mtawa nchini Italia.

Thumb
Mt. Fransisko alivyochorwa na Murillo.

Ametambuliwa na Kanisa Katoliki chini ya Papa Leo X kuwa mtakatifu kuanzia mwaka 1519.

Tarehe ya kifo chake, yaani 2 Aprili, pia ni sikukuu yake[1].

Maisha

Fransisko alizaliwa kwa muujiza katika mji wa Paola, mkoa wa Calabria, Italia, mwaka 1416. Wazazi wake walikuwa wamefikia uzee bila ya kuweza kuzaa, lakini walimuomba Fransisko wa Asizi na kuweka nadhiri kuwa mtoto wao ataitwa Fransisko. Ndipo walipojaliwa kuzaa.

Tangu utotoni alishika maisha magumu ya sala na toba upwekeni.

Alianzisha shirika la watawa wakaapweke, ambalo baadaye likawa Utawa wa Wadogo Kabisa, likapata kibali kutoka kwa Papa mwaka 1506. Pamoja na kuahidi mashauri ya Kiinjili matatu ya kawaida, wanaahidi pia kuishi daima kwa toba kama wakati wa Kwaresima.

Kanuni yake ni ya pekee, ingawa inafuata kwa jumla ile ya Ndugu Wadogo ikiiongezea malipizi makali ya mababu wa jangwani na katazo la kugusa pesa. Badala yake alitaka hao Waminimi waishi kwa kupokea misaada bila kumiliki chochote

Kaulimbiu yake ilikuwa neno "caritas" (kwa Kilatini, "upendo").

Fransisko alifariki mwaka 1507 huko Tours, Ufaransa alipokuwa ametumwa na Papa kwa ombi la mfalme Alois XI aliyemtaka karibu naye wakati wa kufa [2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads