Mataifa ya G20 ya viwanda
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kundi la Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu Ishirini (linalojulikana kama G-20, G20 au Group of Twenty) ni kundi la mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu kutoka nchi zenye uchumi mkubwa duniani: nchi 20, kuongezea Umoja wa Ulaya.
Remove ads

Kwa pamoja, uchumi wa G-20 unajumuisha 85% ya[1] bidhaa jumla zinazotoka katika nchi[1] ulimwenguni, 80% ya biashara duniani (pamoja na biashara ya EU ya ndani) na theluthi mbili ya idadi ya watu duniani.[2]
G-20 ni kama ukumbi wa ushirikiano na kushauriana kuhusu masuala ya mfumo wa fedha wa kimataifa. Husoma, kupitia upya, na kukuza majadiliano kati ya nchi muhimu za viwanda na soko zinazoibukia kuhusu masuala ya sera zinazohusu uendelezaji wa udhibiti wa fedha kimataifa, na hutaka kushughulikia masuala ambayo yako juu ya majukumu ya shirika lolote.!!
Kwa G-20 kuongeza nguvu tangu kongamano la Washington la mwaka 2008, viongozi wake walitangaza tarehe 25 Septemba 2009, kwamba kundi hilo lingechukua pahala pa G8 kama halmashauri kuu ya kiuchumi ya mataifa tajiri.[3]
Viongozi wa mataifa wanachama wa G-20 hukutana kila mwaka mara mbili katika Kongamano la G-20.
Remove ads
Mpangilio
G-20 hufanya kazi bila sekretarieti ya kudumu wala wafanyakazi. Uenyekiti huzunguka kila mwaka kati ya wanachama na huchaguliwa kutoka kwa kambi tofauti za nchi. Mwenyekiti ni mmoja wa memba wa kundi la usimamizi la watatu la zamani, sasa na wenyekiti wa baadaye lifahamikalo kama Troika. Mwenyekiti wa sasa huunda sekretarieti ya muda kwa wakati wake, ambayo inaratibu kazi ya kikundi na kupanga mikutano yake. Jukumu la Troika ni kuhakikisha mwendelezo wa kazi za G-20 na usimamizi katika miaka ijayo. Ifuatayo ni orodha ya nchi wenyekiti wa G-20:[4]
Mwanachama wa 20 ni Umoja wa Ulaya ambao unawakilishwa na Rais wa Baraza la Ulaya na Benki Kuu ya Ulaya
Kuongezea wanachama hawa 20, vikao na taasisi zifuatazo, zikiwakilishwa na maofisa watendaji wakuu, hushiriki katika mikutano ya G-20:
- Shirika la Fedha la kimataifa
- Benki ya Dunia
- Shirika la Fedha na Kamati ya Fedha
- Kamati ya Maendeleo ya IMF na Benki ya Dunia
Remove ads
Uanachama
Uanachama wa G-20 unajumuisha:
- mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa G7, nchi zingine muhimu 12, na Rais wa Umoja wa Ulaya (kama si mwanachama G7)
- Benki Kuu ya Ulaya
- Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa
- Mwenyekiti wa IMF
- Rais wa Benki ya Dunia
- Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo
Uanachama hauonyeshi kabisa nchi 19 zenye uchumi mkubwa duniani katika mwaka. Shirika hili linasema:[5]
“ | kwa ukumbi kama wa G-20, ni muhimu hasa kwa nchi wanachama kuzuiuwa na kufuata kanuni kuhakikisha kuenda vyema na uendelevu kwa shughuli zake. Hakuna vigezo rasmi vya kujiunga na G-20 na mtungo wa kikundi hiki umekuwa haujabadilika tangu kilipoanzishwa. Kwa kuangalia malengo ya G-20, ilifikiriwa ni muhimu kuwa nchi na kanda zenye umuhimu kwenye mfumo wa fedha wa kimataifa zijumuishwe. Mambo kama vile usawa wa Jiografia and kuwakilishwa kwa umma pia yalichangia pakubwa. | ” |
Mataifa yote wanachama 19 ni kati ya chumi bora 32 kama ilivyo pimwa katika Pato la Taifa kwa bei nomino katika orodha iliyochapishwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mwaka 2008.[6] Nchi ambazo hazijawakilishwa katika G-20 ni Uswisi (19), Norway (25), Taiwan (26), Iran (28) na Venezuela (31), hata ingawa wako juu ya orodha kuliko baadhi ya wanachama. Uhispania (9), Uholanzi (16), Poland (18), Ubelgiji (20), Uswizi (22), Austria (24), Ugriki (27) na Denmark (29) wanawakilishwa tu kama memba wa EU, wala si memba kamili. Wakati Pato la Taifa linapimwa kwa viwango vya nguvu za ununuzi (PPP), wanachama wote 19 ni kati ya bora 24 duniani katika mwaka 2008, kulingana na IMF.[7] Iran (17), Taiwan (19) na Thailand (23) si wanachama wa G-20, huku Uhispania (12), Uholanzi (19) na Poland (20)wakijumuishwa tu katika kipengele cha EU. Hata hivyo, katika orodha ya wastani wa Pato la Taifa, iliyokadiriwa kwa miaka tangu kuundwa kwa kundi hili (1999-2008) kwa viwango vyote vya nomino na vya PPP, Uhispania, Uholanzi, Taiwan, na Poland tu ndiyo wanaonekana juu ya mwanachama yeyote wa G-20 katika orodha zote mbili mtawalia.[8]
Mara nyingi inasemekana kwamba G20, ingawa inatoa uwakilishi mpana zaidi kuliko G8, haina haki ya kufanya maamuzi yanayoathiri dunia nzima, kwa sababu wanachama wake wanachaguliwa bila kanuni zozote. G20 haina mkataba na mijadala yake si ya faraghani, hivyo kuifanya "taasisi isiyo yakidemokrasia." [9] Wakosoaji wanapendekeza mbadala kama vile Baraza la Usalama wa Kiuchumi katika Umoja wa Mataifa, ambapo wajumbe wanapaswa kuchaguliwa na Mkutano Mkuu kufuatia umuhimu wao katika uchumi wa dunia na mchango walio tayari kutoa kwa maendeleo ya uchumi wa dunia.[10]
Remove ads
Historia

G-20, ambayo ilichukua pahala pa G-33, ambayo pia ilikuwa imechukua pahala pa G22, ilitajwa katika mkutano wa G7 mjini Cologne mnamo Juni 1999, lakini ilianzishwa rasmi katika Mkutano wa G7 wa mawaziri wa fedha mnamo tarehe 26 Septemba 1999. Mkutano wa uzinduzi ulifanyika mnamo tarehe 15-16 Desemba 1999 mjini Berlin. Mwakani 2008 Uhispania na Uholanzi waliongezwa kwa mwaliko wa Ufaransa katika Mkutano wa G-20 wa Viongozi kuhusu masoko ya fedha na Uchumi Duniani.
Mnamo 2006, kaulimbiu ya mkutano wa G-20 ilikuwa "Kujenga na Kuendeleza mafanikio. Masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na mageuzi ya ndani ili kufikia "ukuaji endelevu", nishati ulimwenguni na masoko ya rasilimali, 'marekebisho' ya Benki ya Dunia na IMF, na athari za mabadiliko demografiki kutokana na idadi ya wanaozeeka. Trevor A. Manuel, Mbunge, Waziri wa Fedha, Afrika ya Kusini, alikuwa mwenyekiti wa G-20 wakati wa Afrika ya Kusini ilikuwa mwenyeji wa Sekretarieti ya mwaka 2007. Guido Mantega, Waziri wa Fedha, Brazili, alikuwa mwenyekiti wa G-20 mwaka 2008; Brazili ilipendekeza mazungumzo juu ya ushindani katika masoko ya fedha, nishati safi na maendeleo ya kiuchumi na vipengele vya fedha vya ukuaji na maendeleo. Katika taarifa kufuatia mkutano wa G7 mawaziri wa fedha tarehe 11 Oktoba 2008, Rais wa Marekani George W. Bush alisema kuwa mkutano ujao wa G-20 utakuwa muhimu katika kutafuta jawabu la (uliyoitwa kwa wakati huo) mgogoro wa kiuchumi wa 2008. Mpango wa Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown ulipelekea kuweko kwa mkutano maalum wa G-20, Kongamano la Viongozi wa G-20 kuhusu masoko ya fedha na uchumi wa dunia, mnamo tarehe 15 Novemba 2008.[11] Viongozi wa G20 walikutana tena mjini London mnamo tarehe 2 Aprili 2009.[12] Kongamano lingine la G20 yalifanyika mnamo 24-25 Septemba 2009 mjini Pittsburgh, Pennsylvania. [13]
Mikutano ya G-20
Kongamano la G-20 lilianzishwa kama itikio kwa tatizo wa kifedha la 2007-2010 na pia kwa kuonekana kwamba nchi zinazostawi hazikuwa zimejumuishwa vya kutosha katika majadiliano ya kiuchumi duniani na utawala. Makongamano ya G-20 ya wakuu wa nchi au serikali yalifanyika mbali na Mikutano ya G-20 ya Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu ambao waliendelea kukutana kuandaa Kongamano la wakuu wa nchi na pia kutekeleza maamuzi yao.
Mikutano ya Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu:
|
|
|
Mmenyuko wa Umma
Tangu mwaka 1999, G-20 mikutano mingi ya G-20 imekuwa ikipingwa. Maandamano mengi huanza kwa amani, lakini mingi hugeuka vurugu na watu wengi hujeruhiwa na uharibifu wa mali katika maeneo ya mitaa. Sababu hasa za maandamano hubadilika kutoka mkutano hadi mwingine, na hata maandamano mengi wakati wa mkutano mmoja. Hata hivyo, hisia tele na kuguna kwa waandamanaji hakujabadilika. Kama ilivyodhahiri,ukweli ni kwamba maandamano hayo yamekuwa yakiendelea tangu mwaka 1999, na yamendelea kuisha kwa vurugu. Habari zaidi kuhusu maandamano ya mikutano hasa inaweza kupatikana kwenye kurasa za mikutano hiyo katika sehemu ya Angalia Pia.:
Remove ads
Angalia Pia
.:
Maelezo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads