Sokwe (Hominidae)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Sokwe (Hominidae)
Remove ads

Sokwe mkubwa (au sokwe tu) ni jina linalounganisha binadamu na nyani wakubwa wa familia Hominidae wanaofanana sana na binadamu. Tofauti na nyani wengine ni kutokuwepo kwa mkia; karibu nyani wote huwa na mkia lakini masokwe wakubwa hawana kabisa. Binadamu (Homo) anahesabiwa pia kama jenasi yenye spishi moja katika familia hii.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Eneo na uenezaji

Masokwe wasiokuwa wanadamu wanaishi katika maeneo ya tropiki ya Afrika (masokwe mtu na ngagi) na Asia (orangutanu). Wote ni wakazi wa misitu ila tu masokwe mtu wanaoingia pia kwenye mbuga au savana. Wanadamu wanaishi duniani kote kwa kubadili mazingira yao, kuvaa nguo na kujenga makazi yanayowalinda kutoka joto kali ama baridi.

Mwainisho

Remove ads

Spishi zilizokwisha

  • Ankarapithecus meteai (Mwisho wa Miocene ya Uturuki)
  • Ardipithecus kadabba (Mwisho wa Miocene ya Uhabeshi)
  • Ardipithecus ramidus (Mwanzo wa Pliocene ya Uhabeshi)
  • Australopithecus afarensis (Pliocene ya Kenya, Tanzania na Uhabeshi)
  • Australopithecus africanus (Pliocene ya Afrika Kusini)
  • Australopithecus anamensis (Pliocene ya Kenya na Uhabeshi)
  • Australopithecus bahrelghazali (Pliocene ya Chadi)
  • Australopithecus garhi (Mwisho wa Pliocene ya Uhabeshi)
  • Australopithecus sediba (Pleistocene ya Afrika Kusini)
  • Gigantopithecus bilaspurensis (Mwisho wa Miocene ya Pakistani na Uhindi)
  • Gigantopithecus blacky (Kati ya Pleistocene ya Uchina)
  • Gigantopithecus giganteus (Pliocene ya Uhindi na Uchina)
  • Kenyanthropus platyops (Kati ya Pliocene ya Kenya)
  • Lufengpithecus chiangmuanensis (Miocene ya Uchina)
  • Lufengpithecus keiyuanensis (Miocene ya Uchina)
  • Lufengpithecus lufengensis (Miocene ya Uchina)
  • Lufengpithecus yuanmouensis (Miocene ya Uchina)
  • Nakalipithecus nakayamai (Mwisho wa Miocene ya Kenya)
  • Oreopithecus bambolii (Miocene ya Italia na Afrika ya Mashariki)
  • Orrorin tugenensis (Mwisho wa Miocene ya Kenya)
  • Ouranopithecus macedoniensis (Mwisho wa Miocene ya Ugiriki)
  • Paranthropus aethiopicus (Mwisho wa Pliocene ya Uhabeshi na Kenya)
  • Paranthropus boisei (Pliocene na Pleistocene za Kenya na Tanzania)
  • Paranthropus robustus (Pleistocene ya Afrika Kusini)
  • Sahelanthropus tchadensis (Mwisho wa Miocene ya Chadi)
  • Sivapithecus indicus (Kati ya Miocene ya Uhindi)
  • Sivapithecus parvada (Kati ya Miocene ya Uhindi)
  • Sivapithecus sivalensis (Kati ya Miocene ya Pakistani na Uhindi)

Picha

Ukweli wa haraka
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sokwe (Hominidae) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads