Masokwe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Masokwe (wingi wa sokwe) ni wanyama wa familia ya juu Hominoidea.
Kuna familia mbili za masokwe: Hylobatidae (masokwe wadogo au giboni) na Hominidae (masokwe wakubwa wakiwemo binadamu).
Masokwe wadogo huishi daima mitini na huteremka kwa nadra. Wana mikono mirefu ili kining'inia kutoka tawi moja hadi jingine na kutoka mti mmoja hadi mwingine. Wanatokea misitu ya tropiki ya Asia.
Masokwe wakubwa hupitisha muda pengine mrefu ardhini, orangutanu muda kidogo tu na ngagi muda mrefu sana. Takriban spishi zote zinatokea Afrika lakini orangutanu wanatokea Asia ya Mashariki.
Remove ads
Uainisho
Familia ya juu Hominoidea (Masokwe)
- Familia Hylobatidae (Masokwe wadogo)
- Familia Hominidae (Masokwe wakubwa)
Remove ads
Picha
- Lar gibbon
- Hoolock gibbon
- Siamang
- Golden-cheeked crested gibbon
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads