Mayotte
département ya Ufaransa From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mayotte ni eneo la ng’ambo la Ufaransa (kwa Kifaransa: Départment de Mayotte). Linaundwa na visiwa vya Maore na Pamanzi pamoja na vingine vidogo. Eneo hili kijiografia ni hasa muungo wa funguvisiwa la Komori lakini si kisiasa. Mayotte iko katika kaskazini ya Mfereji wa Msumbiji kwenye Bahari Hindi, kati ya Madagaska upande wa mashariki-kusini na Msumbiji bara upande wa magharibi. Iko kilometa 295 magharibi kwa Madagaska na km 67 kusini mashariki mwa Nzwani.Ina eneo la takriban km² 374. Ni mwamba wa matumbawe. Mji mkuu ni Mamoudzou tangu mwaka 1977. Mji mkuu wa zamani ni Dzaoudzi kwenye kisiwa cha Pamanzi.
Remove ads
Historia

Mayotte inaonekana kuwa imekaliwa na watu kutoka karne ya 7, wakitokea Madagaska, wengine wenye asili ya Asia na wengine wenye asili ya Afrika.
Kati ya karne ya 8 na karne ya 11 wakazi walisilimu, na kuna msikiti mkongwe (katika Tsingoni) wa karne ya 14, pamoja na mirhab ya matumbawe (1532). Visiwa vyote vya Komori vinafuata utamaduni wa Kiswahili vikiwa pamoja na Mayotte.
Mwaka wa 1841, wakati idadi ya watu ilipungua kwa wakazi chini ya 3000, sultani wa mwisho Andriansoly (kutoka Madagaska) aliuza kisiwa kwa Ufaransa kwa kubadilishana ya ulinzi wa nchi hiyo, hivyo Mayotte ikawa koloni la Kifaransa.
Mwaka 1974, wakati visiwa vingine vitatu vya Komori walidai uhuru na kuunda Umoja wa Komori, Mayotte iliomba kubaki na Ufaransa, na mwaka 2011 ilipewa hali ya eneo la ng'ambo la Ufaransa kwa kura ya maoni.
- Ziara ya Polé (karne XV – XIX).
- Kaburi la Kiswahili sawa na yale ya Lamu.
- Dzaoudzi katika 1855.
- Bendera ya eneo la Mayotte.
Remove ads
Lugha na dini
Kuna lugha tatu ambazo huzungumzwa kisiwani Mayotte, yaani Kifaransa (lugha rasmi), Kimaore ya Komori (55.1%), na Kibushi ya Madagaska.
Utalii
Kisiwa cha Mayotte kina mchanga wa pwani ya rangi tofauti (nyeusi, kahawia, kijivu, nyekundu, beige, nyeupe). Rasi yake ni kubwa (km² 1500).
- Mchanga wa Mstamboro
- Mpito wa Longogori
- Mchanga wa Tsohole
- Nyamba
- Ziwa Dziani
Usafiri

Tazama pia
- Jiografia ya Mayotte
- Watu wa Mayotte
- Siasa ya Mayotte
- Uchumi wa Mayotte
- Mawasiliano ya Mayotte
- Maeneo ya ng’ambo ya Ufaransa
- Wizara za serikali ya Ufaransa
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads