Mutula Kilonzo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Mutula Kilonzo (2 Julai 194827 Aprili 2013) alikuwa mwanasiasa na Wakili Mkuu wa Kenya. Alihudumu kama Waziri wa Elimu, baada ya hapo awali kushikilia wizara ya Nairobi Metropolitan na Sheria na Masuala ya Katiba.[1]

Alikuwa mwanachama wa chama cha Orange Democratic Movement-Kenya (ODM-Kenya) ambacho sasa kinajulikana kama Wiper Democratic Movement. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2013, alichaguliwa kuwa Seneta wa Kaunti ya Makueni.[2]

Remove ads

Maisha Ya Awali Na Elimu.

Mutula Kilonzo alizaliwa na Wilson Kilonzo Musembi na Rhoda Koki Kilonzo. Alikuwa mtoto wa pili katika familia yao. Huyu mtoto mdogo alilazimika kurudia darasa la kwanza kutokana na kukosa shilingi kumi na tano za ada ya shule.[3]

Kilonzo alisoma katika Shule ya Msingi ya Mbooni na Shule ya Machakos kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1969, ambapo alihitimu kwa Shahada ya Sheria ya Heshima ya Kwanza – Shahada ya kwanza katika eneo la Afrika Mashariki.[4]

Remove ads

Safari Ya Kisiasa

Katika Bunge la Taifa la Kenya katika uchaguzi wa bunge wa Desemba 2007, Mutula Kilonzo alichaguliwa kuwa mbunge. Aliteuliwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mitaa ya Nairobi hadi alipopandishwa cheo kuwa Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba tarehe 4 Mei 2009. Alihudumu kama Waziri wa Elimu hadi Aprili 2013, wakati Rais mpya alipoapishwa.[5]

Kilonzo anajulikana kwa kushinikiza kwa njia ya utata kwa wasichana wa shule kutoshurutishwa kuvaa "sketi za nune" ambazo aliziita za kidhalilishaji.Alishinda kiti cha Seneta cha Makueni mwaka 2013 kwa kumshinda John Harun Mwau.[6]

Remove ads

Safari Ya Kisheria

Mutula Kilonzo alihudumu kama wakili binafsi wa Rais mstaafu Daniel arap Moi. Aliingia kwa mara ya kwanza bungeni kama mbunge mteule wa K.A.N.U mnamo Januari 2003.[7]

Katika uchaguzi wa urais wa 2013, ambapo Uhuru Kenyatta alitangazwa kuwa rais mteule wa Kenya na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Raila Odinga alikata rufaa katika Mahakama ya Juu ya Kenya. Kilonzo alikuwa miongoni mwa mawakili waliokusanywa nRaila Odin kutoa huduma za kisheria na kuandaa maombi ya rufaa. Hata hivyo, maombi hayo yalikataliwa na Mahakama Kuu ya Kenya tarehe 30 Machi 2013[8]

Maisha binafsi

Mutula Kilonzo alitengana na mke wake wa kwanza, ambaye ni mama wa watoto wake Wanza, Kethi Kilonzo, Mutula Kilonzo Jnr, na Michael Musembi, mfanyabiashara. Talaka yao ilijulikana kama kesi maarufu ya Kilonzo na Kilonzo aliwakilishwa na Samuel Kivuitu[9]

Baadaye alioa mke wake wa pili, Nduku Musau, ambaye ni binti wa mtaalamu maarufu wa biashara, Musau Mwania kutoka Machakos. Walikuwa na watoto watatu: Muathi Kilonzo, mtaalamu wa fedha, Mutune, na Musau.Mke wake wa kwanza anaishi katika Makazi ya Riara Estate, Nairobi.[10]

Mnamo tarehe 8 Mei 2013, Eunice Nthenya alikubaliwa na mahakama kufanya uchunguzi wa DNA ili kuthibitisha kuwa Mutula Kilonzo alikuwa baba wa mtoto wake, Jackson Muuo, aliezaliwa tarehe 5 Mei 2006. Eunice alidai kuwa walikuwa na uhusiano kati ya mwaka 2005 na 2008. Eunice ni binti wa mlinzi wa Kilonzo, Robert Kavita Malinda.[11]

Remove ads

Kifo.

Mutula Kilonzo alifariki katika shamba lake lilio karibu na nyumba za kulala wageni Maanzoni, iliyo kando ya barabara kuu ya Mombasa, Kaunti ya Machakos, tarehe 27 Aprili 2013[12].

Uchunguzi kuhusu kifo cha Seneta Mutula Kilonzo ulionyesha kuwa hakufa kutokana na shambulio la moyo, bali kuna uwezekano wa sumu kuwa chanzo cha kifo chake. Uvujaji mkubwa wa damu ndani ya mwili wake na kugundulika kwa viungo vyote kuwa salama kulionyesha uwepo wa sumu. Uchunguzi wa mwili ulionyesha kuwa mishipa ya damu na moyo havikuvunjika, jambo linaloonyesha tofauti na hali ya shambulio la moyo, ambapo kawaida mishipa ya damu na moyo huathirika.[13]

Uchunguzi wa maiti ulifanywa na madaktari saba, akiongozwa na mtaalamu mkuu wa serikali wa uchunguzi wa maiti, Dr. Johansen Oduor, na mwenzake Dr. Dorothy Njeru, katika Lee Funeral Home, Nairobi. Mtaalamu wa uchunguzi wa maiti kutoka Uingereza, Calder Ian Maddison, alikusudiwa kwa ombi la familia na alishiriki katika uchunguzi huo. Uchunguzi huu ulishuhudiwa na Seneta wa Machakos, Johnstone Muthama, daktari wa familia, Luke Musau, na Prof. Emily Rogena. Wengine walioshuhudia ni Dr. Frederick Okinyi, mtaalamu wa uchunguzi wa maiti wa serikali wa Machakos (mahali alipofariki), na mtaalamu wa uchunguzi wa maiti wa familia, Andrew Kanyi Gachie.

Mutula Kilonzo alizikwa tarehe 9 Mei 2013 nyumbani kwake katika kijiji cha Woyani, eneo la Utangwa, Kaunti ya Makueni, kulingana na maombi yake. Ibada ya misa ya mazishi ilifanyika tarehe 8 Mei 2013 katika Kanisa la Nairobi Baptist.[14]

Remove ads

Urithi

Mutula Kilonzo alianzisha Mwaki Foundation mwaka 2007 kama sehemu ya juhudi zake za kifadhili na kusaidia jamii. Foundation hiyo ililenga kusaidia na kuleta mabadiliko katika maisha ya watu, hasa katika maeneo ya elimu na maendeleo ya jamii[15][16].

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads