Nyukibambi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Nyukibambi
Remove ads

Nyukibambi (kwa Kiing. bumblebees) ni nyuki wakubwa kiasi wa jenasi Bombus katika family Apidae ya oda Hymenoptera walio na nywele nyingi. Ingawa wana jina la Kiswahili, hawapatikani Afrika kusini mwa Sahara. Wanatokea zaidi Ulaya, Asia na Amerika. Katika Afrika ya Kaskazini, haswa Aljeria, Maroko na Tunisia, kuna spishi 5[1]. Hawa ni nyuki wa kijamii[2] wanaotengeneza viota vyao kwenye machimbo yaliyopo ardhini au matundu mitini au juu ya ardhi kwenye nyasi nzito[3]. Spishi za nusujenasi Psithyrus ni vidusia wa kijamii ambao hunyakua viota vya nyuki wengine ambao wafanyakazi wao hulea majana ya mnyakuzi[4].

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Maelezo

Nyukibambi kwa ujumla wana urefu wa mm 10-25 kulingana na spishi na tabaka[5], ingawa spishi kubwa kabisa, Bombus dahlbomii, inaweza kufikia mm 40 na pengine huitwa panya anayeruka. Ukubwa hutofautiana ndani ya spishi na malkia wa B. terrestris kuwa mm 22, madume mm 16 na wafanyakazi mm 11-17. Nyuki hawa ni imara kuliko nyuki-asali na ncha ya fumbatio yao ni mviringo zaidi. Wana nywele nyingi. Rangi ya kutikulo yao ni nyeusi na nywele nyingi ni nyeusi lakini kuna milia ya nywele za rangi, kwa kawaida nyeupe, njano, machungwa, nyekundu au pinki. Hizi ni rangi za onyo ambazo zinaonyesha kuwa majike wanaweza kutoa mchomo uletao uchungu. Kwa sababu ya ndimi zao ndefu nyukibambi wanaweza kukusanya mbochi kutoka kwa maua ya kina kirefu kuliko nyuki-asali.

Remove ads

Spishi za Afrika

  • Bombus mocsaryi
  • Bombus lapidarius
  • Bombus ruderarius
  • Bombus ruderatus
  • Bombus terrestris

Picha

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads