Olaf II Haraldsson

From Wikipedia, the free encyclopedia

Olaf II Haraldsson
Remove ads

Olaf II Haraldsson (kwa Kinorwe asili: Ólafr Haraldsson; pia Olave; 99529 Julai 1030) alikuwa mfalme wa Norway kuanzia mwaka 1015 hadi 1028.

Thumb
Sarafu ya Mt. Olaf miaka 10231028.
Thumb
Mt. Olaf katika kioo cha rangi dirishani mwa kanisa la Ålesund.

Mtu wa watu, alieneza katika ufalme wake imani ya Kikristo aliyoifahamu huko Uingereza, akapambana na Upagani kwa bidii hadi alipouawa na maadui waliomshambulia kwa upanga huko Stiklestad[1].

Mwaka mmoja baadaye alitangazwa na askofu Grimketel huko Nidaros (Trondheim) kuwa mtakatifu. Jambo hilo lilichangia sana uenezi wa Ukristo nchini, naye akawa kiini cha utambulisho wa taifa[2][3].

Mwaka 1164 Papa Alexander III alithibitisha utakatifu wake.

Pamoja na Wakatoliki na Waorthodoksi[4], baadhi ya Walutheri na Waanglikana pia wanamheshimu hivyo.[5]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Julai[6].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads