Papa Callixtus I

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Callixtus I
Remove ads

Papa Callixtus I alikuwa Papa kuanzia takriban 218 hadi kifodini chake takriban 222[1].

Thumb
Papa Kalisto I.

Alimfuata Papa Zefirino akafuatwa na Papa Urbano I.

Aliwahi kuwa mtumwa[2], lakini mwaka 199 Papa Zefirino alimfanya shemasi na mshauri wake mkuu.

Baada ya kuishi kirefu uhamishoni huko Sardinia, aliwajibika kutunza shamba la Mungu kwenye barabara Appia ambalo sasa lina jina lake mwenyewe: huko alikusanya masalia ya wafiadini, yaweze kuheshimiwa na watu wa nyakati zijazo[3].

Kisha kuchaguliwa kuwa Papa, pamoja na kutetea imani sahihi, kwa upole wake alipatanisha na Kanisa walioasi akafaulu pia kuvuta wafuasi wa uzushi na mafarakano mbalimbali, akifundisha kwamba Kanisa lina mamlaka ya kusamehe dhambi zote. [4][5] Kutokana na msimamo huo, inasemekana waliokuwa wakali zaidi walimchagua Hipoliti wa Roma kama antipapa wa kwanza.[6]

Uongozi wake bora ulifikia kilele chake kwa kufia dini.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 14 Oktoba, alipozikwa katika shamba la Mungu kwenye barabara Aurelia [7].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Maandishi yake

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads