Papa Paulo I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Paulo I alikuwa Papa kuanzia mwezi Aprili au tarehe 29 Mei 757 hadi kifo chake tarehe 28 Juni 767[1]. Alitokea Roma, Lazio, Italia[2] katika familia Orsini[3] [4].

Alimfuata Papa Stefano II ambaye alikuwa kaka yake, akafuatwa na Papa Stefano III.
Kabla ya kuteuliwa Papa alikuwa shemasi na kutumwa na kaka yake kupatana na Walombardi waliotawala sehemu kubwa ya Italia. Alichaguliwa ili kuendeleza sera hiyo, naye alijitahidi kutetea haki za Kanisa kwa msaada wa mfalme wa Wafaranki, Pipino Mfupi, ingawa kwa kufanya hivyo alimchukiza kaisari wa Dola la Roma Mashariki[5].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads