Warangi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Warangi
Remove ads

Warangi ni mojawapo kati ya makabila yanayopatikana katika wilaya ya Kondoa, mkoa wa Dodoma, mji ambao ndiyo makao makuu ya nchi ya Tanzania.

Thumb
Mwanamke Mrangi akioka chapati kwa hoteli yake.

Kirangi ndiyo hasa lugha ya Warangi, ambayo wao huiita Kilaangi.

Warangi wamegawanyika katika dini ya Uislamu na Ukristo, hasa wa Kanisa Katoliki.

Asili na uenezi

Ni kati ya makabila yaliyotokea Mijikenda (leo nchini Kenya). Inasemekana Warangi ni kabila lenye asili ya Ethiopia yaani Wakushi wa Kusini. Waliweza kuhamia Tanzania kutoka Ethiopia mnamo miaka ya 1700[1].

Hadi leo, kwa muonekano Warangi wanafanana na Wahabeshi kuwa wana sura nyembamba, pua ndefu na nywele za kuchanganya asili ya Asia na Afrika.

Mwaka 1999 idadi ya Warangi ilikadiriwa kuwa 350,000. .

Remove ads

Utamaduni

Kuhusu utamaduni wa Warangi, kijitabu kimetolewa juu ya vifaa vya zamani, kama kirindo, kyome kipekecho na vinginevyo.

Chakula kikuuu cha Warangi ni ugali wa mahindi au uwele, na mboga zinazotumika ni kama vile maziwa(masusu), kirumbu (mlenda) na nyama.

Pia Warangi hujishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara; mazao ya chakula ni kama uwele, mtama, mahindi n.k. na mazao ya biashara ni kama vile karanga, alizeti, njugu mawe na kunde.

Vazi rasmi la kabila hili ni kaniki, lakini wengi wanavaa mavazi ya Kiarabu yakiwemo hijjab, kanzu na n.k.

Kuhusu ngoma, kuna ngoma kama mdundiko wa Kirangi ambao huchezwa na watu wa kabila hilo, mara nyingi ukiwa mchana.

Majina mara nyingi huendana na wakati uliopo, kwa mfano: Mwasu (jua), Mbula (mvua), Nchira (ngozi), Nyange, Ndudya, Kichiko (masika), Salala (kimvua kidogo), Mnjira, Kifuta, Mwapwani, Ichuka, Luji, Kidunda n.k.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads