Woodrow Wilson

Rais wa Merika kutoka 1913 hadi 1921 From Wikipedia, the free encyclopedia

Woodrow Wilson
Remove ads

Thomas Woodrow Wilson (28 Desemba 18563 Februari 1924) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Marekani.

Ukweli wa haraka 28 Rais wa Marekani, Makamu wa Rais ...
Thumb
Remove ads

Mtaalamu na profesa

Alizaliwa Staunton, Virginia akiwa mtoto wa mchungaji wa Kanisa la Kipresbiteri.

Alisoma sheria na historia kwenye vyuo vikuu vya Princeton na Johns Hopkins kule Baltimore, Maryland. Alifundisha kwenye vyuo mbalimbali hadi kuwa profesa wa Chuo Kikuu cha Princeton mwaka 1890 na mkuu wa chuo mwaka 1902.

Mwaka 1910 alijiunga na siasa akachaguliwa gavana wa New Jersey. Mwaka 1912 aligombea urais wa nchi kwa chama cha Democratic Party akashinda.

Remove ads

Rais wa Marekani

Miaka ya 1913 hadi 1921 alikuwa Rais wa Marekani akiwa rais wa kwanza kutoka majimbo ya kusini tangu vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani.

Katika siasa yake alipunguza kodi nyingi, aliunda benki kuu ya taifa na kuweka mipaka kwa athira ya makampuni makubwa yaliyowahi kusimamia soko kwa mapatano kuhusu bei ya bidhaa na hivyo kuzuia makampuni mapya. Alifaulu kupitisha sheria iliyoanzisha muda wa kazi kuwa saa nane kwa siku. Alianzisha pia mfumo wa kusaidia wakulima.

Hakupenda makoloni ya Marekani yaliyokuwa hasa Ufilipino na Puerto Rico, hivyo alichukua hatua za kukabidhi madaraka kadhaa kwa wazalendo akaandaa uhuru wa Ufilipino uliofuata miaka 30 baadaye.

Alipunguza haki kadhaa ya Waamerika Weusi. Aliita mawaziri kutoka majimbo ya kusini akawaruhusu kutenganisha Wamarekani Weupe na Weusi katika idara zao[1][2][3][4][5][6]. Katika idara hizo ofisi, vyoo na vyumba vya kula vilitenganishwa kufuatana na rangi ya wafanyakazi. Wilson aliendelea kuteua Weusi kadhaa kuwa na nafasi ya uongozi katika idara za serikali lakini alipunguza idadi ya nafasi hizo.

Wakati wa vita, Wamarekani Weusi wengi waliitwa kuwa wanajeshi, wakapata malipo sawa na wote wengine lakini walipangwa katika "vikosi vyeusi" ambamo askari Weusi walihudumia chini ya maafisa Wazungu.

Remove ads

Rais wakati wa Vita Kuu ya Kwanza

Mwaka 1917 Marekani iliingia katika Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza dhidi ya Mataifa ya Kati (Central Powers: Ujerumani, Austria-Hungaria na Milki ya Osmani) baada ya meli za Marekani kuzamishwa na nyambizi za Ujerumani na jaribio la Ujerumani kuchochea Meksiko dhidi ya Marekani. Mchango wa Marekani ulihakikisha ushindi wa Mataifa ya Ushirikiano (Allied Powers: Ufaransa, Uingereza, Italia, Marekani).

Hata hivyo, Wilson alijaribu kufikia aina ya amani iliyoepuka masharti makali dhidi ya washindwa wa vita, pamoja na kukubali haki ya mataifa ya kujiamulia wenyewe. Hapo hakufaulu katika Mkataba wa Versailles lakini aliweza kuanzisha Shirikisho la Mataifa Kutokana na upinzani wa Ufaransa na Italia kama ushirikiano wa mataifa kwa shabaha ya kuzuia vita tena. Kwa jitihada zake alipewa Tuzo ya Nobel ya Amani kwenye mwaka 1919.

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads