Maryland

From Wikipedia, the free encyclopedia

Maryland
Remove ads

Maryland ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Imepakana na majimbo ya Pennsylvania, West Virginia, Delaware, Virginia na mkoa wa shirikisho la Washington DC.

Thumb
Sehemu ya Jimbo la Maryland
Ukweli wa haraka Nchi, Mji mkuu ...
Thumb
Ramani ya Maryland

Iko kwenye pwani ya Atlantiki upande wa mashariki wa Marekani bara. Hori ya Chesapeake inagawa eneo la jimbo pande mbili.

Mji mkuu ni Annapolis na mji mkubwa ni Baltimore. Kwa miji mingine, angalia orodha ya miji.

Remove ads

Historia

Iliundwa kama koloni la Uingereza mwaka 1634 na kabaila Lord Baltimore aliyetumia jina la Maryland kwa heshima ya mke wa mfalme Charles I. Baltimore aliyetoka Eire alitafuta hasa mahali kwa ajili ya Wakatoliki wasiokubaliwa katika makoloni mengine ya Uingereza. Maryland ilikuwa koloni la kwanza lenye sheria iliyokubali madhehebu yote ya Kikristo.

Mji mkuu wa Washington DC ulijengwa kwenye eneo lililotengwa na eneo la Mayrland kando ya mto Potomac.

Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani (1861-1865) Maryland ilikaa upande wa Maungano.

Remove ads

Viungo vya Nje

Ukweli wa haraka


Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Maryland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads