Yohane Baptista de La Salle
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Yohane Baptista de la Salle (kwa Kifaransa: Jean-Baptiste de La Salle; Reims, Ufaransa, 30 Aprili 1651 - Saint-Yon, Rouen, Ufaransa, 7 Aprili 1719) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mlezi wa vijana wengi, hasa fukara, ambaye kwa ajili ya malezi yao ya kiutu na ya Kikristo alianzisha pia kwa tabu nyingi shirika la Mabradha wa Shule za Kikristo[1].



Anahesabiwa mwanzilishi wa shule Katoliki duniani. De La Salle anahesabiwa pia kuwa wa kwanza kuendesha chuo cha ualimu (1685).
Remove ads
Maisha
Akifuata njia ya upadri tangu utotoni, alimaliza masomo na kupata upadirisho tarehe 9 Aprili 1678.
Miaka miwili baadaye alipata udaktari wa teolojia.
De La Salle aliingia kazi ya malezi taratibu, bila ya kukusudia, kadiri ya matukio na watu aliokutana nao.
Juhudi zake za kuanzisha shirika la mabradha tu kwa ajili ya kuendesha shule zilipata upinzani mkubwa kwa sababu ulikuwa mpango mpya.
Pia mbinu zake zilikuwa hazijazoeleka, kama vile kutumia lugha ya kawaida na kutodai ada yoyote.
Hata hivyo alifaulu kuanzisha mtandao wa shule nchini Ufaransa.
Remove ads
Heshima baada ya kifo
Alitangazwa na Papa Leo XIII kuwa mwenye heri tarehe 19 Februari 1888 na mtakatifu tarehe 24 Mei 1900.
Papa Pius XII alimtangaza msimamizi wa walimu wote tarehe 15 Mei 1950.
Athari yake
Kazi yake ilienea haraka. Leo duniani shirika lake lina mabradha 2,883 (mbali ya walei na watawa zaidi ya 100,000 wanaoshiriki kazi yao) wanaolea vijana kama 1,160,000 katika vituo vya malezi 1,154 vya nchi 78.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads