Addai
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Addai, kwa Kiaramu ܐܕܝ,[1] ni mtakatifu anayeheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo, hasa wa Mashariki, ingawa hakuna makubaliano ya wanahistoria kuhusu maisha yake.
Remove ads
Masimulizi juu yake
Kadiri ya mapokeo, hasa ya kitabu Mafundisho ya Addai, alikuwa Myahudi mzaliwa wa Edessa, wakati ule sehemu ya Syria, siku hizi nchini Uturuki.
Alipokwenda kuhiji Yerusalemu, alimsikiliza Yohane Mbatizaji na kubatizwa naye katika mto Yordani, akabaki Palestina.
Baadaye akawa mfuasi wa Yesu, akachaguliwa naye kati ya wanafunzi 70 kwenda kuhubiri wawiliwawili.
Baada ya ufufuko wa Yesu na Pentekoste ya mwaka uleule, Addai alianza kuhubiri Injili huko Mesopotamia, Syria na Persia.
Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Agosti, pamoja na mwanafunzi wake Mari.
Hata leo inatumika anafora yenye majina yao isiyo na simulizi la Karamu ya mwisho, tofauti na nyingine zote.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads