Elisha

From Wikipedia, the free encyclopedia

Elisha
Remove ads

Elisha (kwa Kiebrania אֱלִישַׁע, Elisha, yaani "Mungu wangu ni wokovu", kwa Kigiriki Ἐλισσαῖος, Elissaios au Ἐλισαιέ, Elisaie, kwa Kiarabu الْيَسَع Elyasaʿ) alikuwa nabii anayetajwa katika Biblia na katika Qur'an.

Thumb
Elisha katika Promptuarii Iconum Insigniorum.
Thumb
Picha ya Elisha (karne ya 18, kwenye monasteri ya Kizhi, Russia).
Thumb
Elisha akimfufua mtoto wa mwanamke Mshunami katika mchoro wa mwanzo wa karne ya 20.

Mwanafunzi wa Elia, ingawa hakuacha maandishi, alitabiri wokovu ujao wa mataifa yote kwa miujiza aliyowafanyia watu wasio Waisraeli[1].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Juni[2][3].

Remove ads

Katika Biblia

Elisha alifanya unabii wake katika ufalme wa kaskazini wa Israel wakati wa wafalme Yoram, Yehu, Yehoahaz na Yehoashi [4]

Elisha alikuwa mwana wa Shaphat kutoka Abel-meholah aliyepata kuwa mfuasi wa nabii Elia (Kitabu cha kwanza cha Wafalme 19:16–19).

Baada ya huyo kuchukuliwa mbinguni katika upepo wa kisulisuli (Kitabu cha pili cha Wafalme 2:9), Elisha alikubaliwa kama mkuu wa wanafunzi wake ("wana wa manabii") akajulikana nchini kwa karama zake, zikiwa ni pamoja na uponyaji.

Kwa miaka karibu sitini (892832 hivi KK) alikuwa nabii (2Fal 5:8), akijihusisha sana na siasa akaombwa shauri na wafalme mbalimbali hata wa nchi za nje. Kwa kumpaka mafuta Yehu alianzisha mapinduzi dhidi ya ukoo wa Ahabu na kukomesha upotoshaji wake wa imani. Mapinduzi hayo yakaenea kusini kwa kumuua Atalia, binti wa Yezebeli, aliyetawala miaka saba kisha kuua watu wote wa ukoo wa Daudi (mtoto Yoashi tu alinusurika).

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads