Jokate Mwegelo

Mwigizaji na mjasiriamali wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia

Jokate Mwegelo
Remove ads

Jokate Mwegelo (alizaliwa 20 Machi 1987) ni mwigizaji wa filamu, mjasiriamali na mwanasiasa kutoka nchini Tanzania. Mnamo mwezi Julai 2018 aliteuliwa na rais John Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Ukweli wa haraka Amezaliwa, Utaifa ...

Mnamo mwaka 2006 alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika shindano la Miss Tanzania akiwa nyuma ya Wema Sepetu ambaye alishika nafasi ya kwanza [1]

Jokate vilevile alikuwa mtangazaji na mwimbaji[2][3][4][5] na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Kidoti Company.[6][7]

Mwaka 2011, alishinda tuzo ya Zanzibar International Film Festival kama mwigizaji bora wa kike.[8].Mwaka 2017, Mwegelo aliingizwa katika jarida la Forbes katika Forbes 30 Under 30 kutoka Afrika.[9]

Remove ads

Maisha ya awali na elimu

Jokate Mwegelo alizaliwa jijini Washington, D.C., Marekani, ambapo wakati huo wazazi wake walikuwa wanafanya kazi.

Alikulia jijini Dar es Salaam, Tanzania. Alianza elimu ya msingi katika shule ya Olympio Primary School na baadaye St. Anthony High School, halafu Loyola High School, Dar es Salaam.

Alihitimu katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, ambapo alipata shahada ya sayansi ya siasa na falsafa.

Remove ads

Miss Tanzania 2006

Alikuwa mshindi wa pili katika shindano la Miss Tanzania mwaka 2006.[10] Vilevile alipewa jina la balozi wa Redds fashion na balozi wa gazeti la Citizen, baada ya kupata kura nyingi mwaka huo.[5]

Kabla ya Miss Tanzania, alishindana katika Miss Kurasini 2006, shindano ambalo alishinda, kisha kuelekea juu zaidi na kuwa Miss Temeke 2006, ambako pia alishinda.[11]

Kazi

Mwaka 2018 aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Joseph Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe, mwaka 2020 alibadilishwa na kuwa mkuu wa wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Kuigiza

Mwaka wa 2007, alipata kucheza filamu yake ya kwanza iliyojulikana kwa jina la Fake Pastors, akiwa na Vincent Kigosi, Lisa Jensen, mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2006 na marehemu Adam Kuambiana.[12]

Mwaka wa 2008, amecheza katika filamu ya From China With True Love[13]

Mwaka2010, alionekana katika filamu ya Chumo, filamu iliyoandaliwa na Media for Development International, kuhusu elimu juu ya ugonjwa wa malaria.[14] Filamu hii ilimwezesha kupata tuzo ya Zanzibar International Film Festival akiwa kama mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2011 na kuchaguliwa kama mwigizaji wa Pan-Afrika katika tuzo za 2012 Nigeria Entertainment Awards.

Vilevile amepata kuonekana katika mfululizo wa tamthilia maarufu kwa jina Siri Ya Mtungi, iliokua imendaliwa na Jordan Riber na kuongozwa na Karabani, mnamo mwaka 2013.[15] Mwaka wa 2014, amecheza uhusika wa "Ndekwa" katika filamu ya Mikono Salama, ambayo ilimpelekea apate tuzo nyingine ya Zanzibar International Film Festival akiwa mwigizaji bora wa kike kwa filamu za Kiswahili.[16]

Remove ads

Kampuni ya Kidoti

Muziki

Alishirikishwa katika wimbo wa Japo Nafasi wa Cpwaa akiwa na A.Y. katika wimbo wa Kings and Queen, na Amani, kutoka Kenya. Mwaka wa 2013, alitoa wimbo wake akiwa na Lucci, uliyoitwa 'Kaka na Dada.[17][18] Mwaka wa 2015, akadondosha wimbo wake mwingine uliyoitwa Leo akiwa na mwimbaji mwingine kutoka nchini Nigeria maarufu kama Ice Prince.[19]

Siasa

Jokate hakujulikana kujishughulisha na siasa hadi mwaka 2017 alipoteuliwa na Umoja wa Vijana wa chama cha CCM (UVCCM) kuongoza Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi ya umoja huu akiwa kaimu katibu wa idara hii. Yeye mwenyewe alitaja maarifa ya utoto wake alipohamasishwa na bibi yake aliyekuwa mwasisi wa Umoja wa Walimu Tanzania katika Mkoa wa Rukwa kuona ni muhimu kujitoa katika jamii na kuchukua nafasi za uongozi. [20] Wakati ule magazeti yalileta taarifa kuwa uteuzi wake ulipingwa na sehemu ya viongozi wa umoja huu.[21]

Kwenye mwezi wa Machi 2018 aliondolewa katika nafasi hii kwa azimio la kamati kuu ya UVCCM.[22]

Mwisho wa mwezi wa Julai 2018 aliteuliwa na rais Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe[23], uteuzi ambao ulileta cheche nyingi katika uwanja wa mitandao nchini Tanzania. Wapo waliobeza uteuzi huo, wapo waliosifia. Wengine waliweka picha zake za zamani zilizokuwa hazina maadili ili kukebehi uteuzi huo.

Remove ads

Filamu

  • Movies
Maelezo zaidi Mwaka, Filamu ...
  • Mfululizo wa TV
Maelezo zaidi Mwaka, Mfululizo ...
Remove ads

Diskografia

  • 2013

Kaka Dada akiwa na Lucci

  • 2015

Leo Leo akiwa Ice Prince

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads