Jivu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Jivu ni mabaki ya poda hafifu yanayotokana na uchomaji wa vitu vya kikaboni kama vile kuni, makaa, mimea au taka nyingine. Kwa asili, jivu huundwa na oksidi za metali, chumvi na madini yasiyoweza kuungua, miongoni mwake calcium, potassium na phosphorus. Rangi ya jivu hubadilika kulingana na chanzo na hali ya moto, ikianzia kijivu chepesi hadi jeupe au hata jeusi. Katika mazingira ya kilimo, jivu hutumika kurutubisha udongo kwa sababu lina virutubishi vinavyoongeza rutuba na kurekebisha asidi ya ardhi.

Remove ads
Majivu katika Biblia
Tamari alipobakwa na kaka yake, alijimwagia majivu kichwani, akararua nguo yake akaficha uso wake mikononi mwake akilia hadharani (2 Sam 13:19).
Nabii Yeremia alipohimiza toba, alisema: "Binti wa watu wangu, jivike gunia, jizungushe majivuni" (Yer 6:26).
Ayubu alipotokewa na Mungu alimjibu: "Nilikuwa nimesikia habari zako, lakini sasa nimekuona. Ndiyo sababu najichukia na kutubu katika mavumbi na majivu" (Ayu 42:5–6).
Kitabu cha Yona (Yon 3:6) inasimulia kwamba baada ya nabii huyo kutisha wakazi wa Ninawi, wao walifunga chakula na maji pamoja na kuvaa majivu na magunia.[1] Hapo Mwenyezi Mungu aliwasamehe.[1]
Nabii Danieli alisimulia: "Nilimgeukia Bwana Mungu, nikimsihi kwa sala nyofu, kwa saumu, gunia, na majivu" (Dan 9:3).
Wamakabayo walipokwenda kupigana kwa ajili ya uhuru wa taifa la Israeli walijiandaa hivi: "Siku hiyo walifunga na kuvaa gunia; walijimwagia majivu kichwani na kurarua nguo zao" (1 Mak 3:47; taz. 4:39).
Yesu alilaumu watu wa kizazi chake walioshuhudia miujiza yake: "Maajabu yaliyofanyika kwenu yangefanyika huko Tiro na Sidoni, wakazi wake wangewahi sana kutubu kwa gunia na majivu" (Math 11:21; Lk 10:13).
Mifano mingine inapatikana katika Hes 19:9; 19:17; Est 4:1 na Eb 9:13.
Wakristo waliendeleza desturi hiyo ya kutumia majivu kuonyesha toba.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads