From Wikipedia, the free encyclopedia
Maria wa Bethania (jina lake kwa Kiebrania מִרְיָם, Miryām, kwa Kiaramu מרים, Maryām, kwa Kigiriki Μαρία, Maria) alikuwa mwanamke wa Bethania, kitongoji cha Yerusalemu, katika karne ya 1[1].
Ndugu zake walikuwa Martha na Lazaro wa Bethania, ambao wote Yesu alifurahia urafiki wao hasa alipohiji kwenda Yerusalemu.
Wanaheshimiwa na Wakristo wengi kama watakatifu[2].
Sikukuu yao inaadhimishwa pamoja tarehe 29 Julai[3] au 4 Juni, kadiri ya madhehebu.
Anajulikana hasa kutokana na Injili, kwa namna ya pekee Injili ya Luka (10:38-42) na Injili ya Yohane (11; 12:1-8), katika Agano Jipya ndani ya Biblia ya Kikristo.
Humo anaonekana mwenye silika ya utulivu na imani kwa Yesu Kristo, ambaye alipendezwa sana na usikivu wake wakati alimfundisha ameketi chini karibu na miguu yake, kama ilivyokuwa kawaida ya wanafunzi wa dini ya Kiyahudi, ingawa wakati huo wanaume tu walikubalika.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.