Agnes wa Praha

From Wikipedia, the free encyclopedia

Agnes wa Praha
Remove ads

Agnes wa Praha (au wa Bohemia; Praha, leo mji mkuu wa Ucheki, 1211 - Praha, 2 Machi 1282) alikuwa bintimfalme aliyeanzisha na kuongoza kama abesi monasteri ya Kifransisko mjini Praha; alianzisha pia Shirika la Wanamsalaba wa Nyota Nyekundu.

Thumb
Mt. Agnes akiuguza wagonjwa, sehemu ya mchoro wa karne XV.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira, hasa katika tarehe ya kifo chake[1] au tarehe 6 Machi.

Remove ads

Maisha

Binti wa mfalme wa Bohemia Ottokar I na Kostanza wa Hungaria, alikuwa ndugu wa jirani wa watakatifu Ludmila, Wenseslaus I, Hedwig wa Andechs, Elizabeti wa Hungaria na Margareta wa Hungaria.

Kisha kulelewa katika monasteri ya masista wa Citeaux huko Trzebnica, na ya masista Wapremontree huko Doksany, alipokuwa na miaka 8 alitumwa kwenye ikulu ya Vienna ili kuandaliwa awe mke wa kaisari Henri VII wa Ujerumani, mwana wa Federiko II.

Akiguswa na mfano wa Fransisko wa Asizi, aliamua kuishi kitawa na kwa msaada wa Papa Gregori IX alivunja uchumba wake akarudi Praha awe bibiarusi wa Kristo tu.

Huko alianzisha konventi ya kwanza ya Ndugu Wadogo katika eneo hilo (1232), ikiwa pamoja na hospitali kwa fukara: ili kuendesha hospitali hiyo alianzisha chama cha kitume cha Wanamsalaba ambao mwaka 1237 walikubaliwa na Papa kuwa shirika la kitawa.

Mwaka 1234 alianzisha monasteri ya Waklara iliyopokea masista watano waliotumwa na Klara wa Asizi mwenyewe: Agnes alihamia huko tarehe 11 Juni mwaka huohuo akishika kikamilifu ufukara mkuu. Baadaye akawa abesi wake hadi alipofariki dunia [2].

Remove ads

Heshima baada ya kifo

Agnes aliheshimiwa sana mara baada ya kufa: tarehe 28 Novemba 1874 Papa Pius IX alithibitisha heshima hiyo na jina alilopewa tayari la mwenye heri. Tarehe 12 Novemba 1989 Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo kwa Kiswahili

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads