Maria Magdalena

From Wikipedia, the free encyclopedia

Maria Magdalena
Remove ads

Maria Magdalena, yaani wa Magdala (kwa Kigiriki: Μαρία ἡ Μαγδαληνή) ni mmoja kati ya wanafunzi maarufu zaidi wa Yesu wa Nazareti, hasa kutokana na sifa yake ya kuwa mtu wa kwanza kumuona amefufuka (Mk 16:9[1]; Yoh 20:16).

Thumb
Picha takatifu ya Waorthodoksi inayomuonyesha Maria Magdalena akibeba manemane kwa ajili ya kupaka upya maiti ya Yesu.
Thumb
Maria Magdalena chini ya msalaba, akimlilia Kristo aliyekufa.
Thumb
Maria Magdalena akiwa amepiga magoti katika kundi la sanamu maarufu kama Stabat Mater; ni kazi ya Gabriel Wuger, 1868.
Thumb
Maria akiambiwa na mfufuka Noli me Tangere (yaani "Usinishike"); mchoro wa Hans Holbein the Younger, 1524.
Thumb
Yesu na Maria Magdalena (Noli me tangere). walivyochongwa katika karne ya 13.
Thumb
Maria Magdalena alivyochorwa na Ary Scheffer huku akifanya malipizi kadiri ya mtazamo wa karne ya 19.
Thumb
Maria kadiri ya Gheorghe Tattarescu.

Kwa kuwa alitumwa naye kuwapasha habari hiyo Mitume, kuanzia Thoma wa Akwino anaitwa "Mtume wa Mitume"[2].

Thumb
Maria wa Magdala kwenye kaburi tupu anavyoonekana katika dirisha la kanisa la Walutheri la St. Matthew huko Charleston, South Carolina, Marekani.
Thumb
Maria Magdalena alivyochorwa na Anthony Frederick Augustus Sandys, 1860 hivi.
Remove ads

Habari zake kadiri ya Injili

Ni kwamba, kadiri ya Injili, baada ya kushuhudia kifo cha Yesu na mazishi yake (Mk 15:40-16:1; Math 27:56-28:1; Yoh 19:25), upendo na juhudi vilimfanya mwanamke huyo awahi kwenye kaburi lake alfajiri ya siku ya Jumapili. Huko alitokewa na malaika na kuambiwa amefufuka.

Ndiye aliyewapasha habari hiyo mitume wa Yesu kabla hawajaenda kaburini na kulikuta halina maiti.

Baada ya Maria, hao pia walitokewa na Yesu mwenyewe, kuanzia mtume Petro.

Kabla hajaanza kumfuata, Maria alikuwa amepagawa na mapepo saba (Mk 16:9). Alipoponywa na Yesu, alijitolea kumhudumia na mali yake pamoja na wanawake wengine (Lk 8:2).

Remove ads

Habari yake kuu katika Yoh 20

1 Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.

2 Basi, akaenda mbio hadi kwa Petro na yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, "Wamemwondoa Bwana kaburini, na wala hatujui walikomweka."

3 Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine wakaenda kaburini.

4 Wote wawili walikimbia lakini yule mwanafunzi mwingine alikimbia mbio zaidi kuliko Petro, akatangulia kufika kaburini.

5 Alipoinama na kuchungulia ndani, aliona sanda, lakini hakuingia ndani.

6 Simoni Petro naye akaja akimfuata, akaingia kaburini; humo akaona sanda,

7 na kile kitambaa alichofungwa Yesu kichwani. Hicho kitambaa hakikuwekwa pamoja na hiyo sanda, bali kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa mahali peke yake.

8 Kisha yule mwanafunzi mwingine aliyemtangulia kufika kaburini, akaingia pia ndani, akaona, akaaamini.

9 Walikuwa bado hawajaelewa Maandiko Matakatifu yaliyosema kwamba ilikuwa lazima afufuke kutoka wafu).

10 Basi, hao wanafunzi wakarudi nyumbani.

11 Maria alikuwa amesimama nje ya kaburi, akilia. Huku akiwa bado analia, aliinama na kuchungulia kaburini,

12 akawaona malaika wawili waliovaa mavazi meupe, wameketi pale mwili wa Yesu ulipokuwa umelazwa, mmoja kichwani na wa pili miguuni.

13 Hao malaika wakamwuliza, "Mama, kwa nini unalia?" Naye akawaambia, "Wamemwondoa Bwana wangu, na wala sijui walikomweka!"

14 Baada ya kusema hayo, aligeuka nyuma, akamwona Yesu amesimama hapo, lakini asitambue ya kuwa ni Yesu.

15 Yesu akamwuliza, "Mama, kwa nini unalia? Unamtafuta nani?" Maria, akidhani kwamba huyo ni mtunza bustani, akamwambia, "Mheshimiwa, kama ni wewe umemwondoa, niambie ulikomweka, nami nitamchukua."

16 Yesu akamwambia, "Maria!" Naye Maria akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, "Raboni" (yaani "Mwalimu").

17 Yesu akamwambia, "Usinishike; sijakwenda bado juu kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu uwaambie: nakwenda juu kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu."

18 Hivyo Maria Magdalene akaenda akawapa habari wale wanafunzi kuwa amemwona Bwana, na kwamba alikuwa amemwambia hivyo.

Remove ads

Heshima aliyopewa baada ya kufa

Maria Magdalena anahesabiwa mtakatifu katika madhehebu mengi ya Ukristo, akiadhimishwa tarehe 22 Julai[3]. Katika Kanisa la Kilatini Papa Fransisko ameipa hadhi ya sikukuu.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads