Serbia

From Wikipedia, the free encyclopedia

Serbia
Remove ads

Serbia (kwa Kiserbokroatia: Република Србија au Republika Srbija) ni nchi ya Ulaya kwenye rasi ya Balkani.

Ukweli wa haraka


Imepakana na Hungaria, Bulgaria, Romania, Masedonia Kaskazini, Kosovo (au Albania), Montenegro, Bosnia na Herzegovina na Kroatia.

Nchi ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na inatarajia kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Mji mkuu ni Belgrad, wenye wakazi milioni 1,2.

Miji mingine muhimu ni Novi Sad (mji mkuu wa jimbo linalojiendesha la Vojvodina), Niš (mji mkubwa zaidi wa kusini na mashariki mwa Serbia) na Kragujevac katika Serbia sahihi, Priština katika jimbo linalojiendesha la Kosovo (hali si ya uhakika).

Miji mingine mikubwa ni Subotica, Novi Pazar, Pančevo, Zrenjanin, Kraljevo, Kruševac, Leskovac, Smederevo na mingine.

Miji muhimu kihistoria na kiutamaduni (ingawa midogo) ni Sremski Karlovci, Negotin, Vranje, Zaječar na Požarevac.

Remove ads

Historia

Waslavi walihamia Balkani baada ya karne ya 6.

Kati yao, Waserbia waliunda falme mbalimbali mwanzoni mwa Karne za Kati.

Mwaka 1217 Ufalme wa Serbia ulitambuliwa na Roma na Bizanti na mwaka 1346 ulifikia kilele cha ustawi wake kama Dola la Serbia.

Hali hiyo haikudumu muda mrefu, tena katikati ya karne ya 16 eneo lote la Serbia ya leo lilitekwa na Waosmani, ingawa wakati mwingine sehemu yake ilitawaliwa na Dola la Wahabsburg.

Mwanzoni mwa karne ya 19, mapinduzi ya Serbia ilileta ufalme wa kikatiba wa kwanza katika Balkani.

Ufalme huo ulizidi kuenea na baada ya vita vikuu vya kwanza vilivyosababisha vifo vingi vya raia zake, Serbia iliungana na makabila kuanzisha Yugoslavia iliyodumu hadi miaka ya 1990 iliposambaratika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 2006 hata Montenegro ilitengana na Serbia, ila kwa amani.

Mwaka 2008 bunge la jimbo la Kosovo lilijitangazia uhuru.

Remove ads

Watu

Nchi, ukiondoa Kosovo, ina wakazi 7,186,862 kwenye eneo la km² 88.361. Wengi wao wana asili ya Kislavoni.

Upande wa dini 85% ni Waorthodoksi, 5% Wakatoliki, 3% Waislamu, 1% Waprotestanti.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Serbia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads