Yakobo Mdogo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Yakobo Mdogo
Remove ads

Yakobo Mdogo ni jina la mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu. Anaitwa hivyo ili kumtofautisha na mtume mwenzake, Yakobo wa Zebedayo.

Thumb
Picha yake iliyochorwa katika ukuta wa kanisa la Waorthodoksi huko Vladimir, Russia karne ya 12.

Katika Injili anaitwa Yakobo wa Alfayo na kutajwa na Injili ya Mathayo 10:3, Injili ya Marko 3:18, Injili ya Luka 6:15, mbali ya Matendo ya Mitume 1:13.

Kutokana na wingi wa Wayahudi waliotumia jina hilo la babu wa taifa la Israeli, ni vigumu kuelewa kama ndiye Yakobo anayetajwa kama mmoja kati ya nguzo za Kanisa la Yerusalemu aliyekubali pendekezo la Mtume Petro kuhusu suala la tohara kwa wasio Wayahudi wanaoongokea Ukristo na hasa kama ndiye mwandishi wa Waraka wa Yakobo [1].

Kama ndiye, aliuawa Yerusalemu mwaka 62 kwa himizo la kuhani mkuu Anna II.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Mei pamoja na Mtume Filipo [2][3].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads