Yuda Tadei

mmoja wa Mitume Kumi na Wawili wa Yesu; kimapokeo anatambulishwa na Yuda nduguye Yesu From Wikipedia, the free encyclopedia

Yuda Tadei
Remove ads

Yuda Tadei ni jina la mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu, ambalo Injili zinajitahidi kumtofautisha na Yuda Iskarioti, msaliti wa Yesu.

Thumb
Mtume Yuda alivyochorwa na Anthonis van Dyck.
Thumb
Sanamu yake katika Kanisa kuu la Roma.

Habari zake za hakika zinategemea Agano Jipya ambamo anatajwa katika orodha ya Thenashara ambao waliteuliwa na Yesu Kristo kama msingi wa taifa jipya la Mungu wakatumwa naye kuhubiri na kuponya.

Injili ya Yohane tu inaripoti neno lake moja, katika simulizi la karamu ya mwisho, alipomuuliza Yesu imekuwaje atajifunua kwao lakini si kwa ulimwengu (14:22). Yesu alimjibu kwamba yeyote anayempenda atashika neno lake, na Baba atampenda na kufanya maskani yake kwake pamoja na Mwana[1].

Anafikiriwa na wengi kuwa mwandishi wa Waraka wa Yuda, lakini hakuna hakika kwa sababu jina hilo la babu wa Wayahudi wote lilikuwa la kawaida mno.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Oktoba pamoja na Mtume Simoni Mkananayo [2][3].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads