Papa Paskali I

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Paskali I
Remove ads

Papa Paskali I alikuwa Papa kuanzia tarehe 25 Januari 817 hadi kifo chake mnamo Februari/Mei 824[1]. Alitokea Roma, Lazio, Italia[2].

Thumb
Mt. Paskali I.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Paskali Massimi, mwana wa Bonosus[3].

Alimfuata Papa Stefano IV akafuatwa na Papa Eugenio II.

Kabla ya kuchaguliwa Papa alikuwa abati wa monasteri iliyohudumia waliofika mjini Roma kwa hija[4]. Kwa kuwa hakusubiri kupata uthibitisho wa kaisari Pius Mtawa, alimtuma balozi kwake[5] naye akarudi na hati Pactum cum Paschali pontifice, ambamo kaisari alimpongeza, alithibitisha mamlaka ya Papa juu ya Dola la Papa, na kuhakikisha siku za mbele uchaguzi wa Mapapa hautaingiliwa na serikali tena.[6] Wanahistoria wana wasiwasi kuhusu hati hiyo kuwa halisi.[7] Kwa vyovyote, baada ya Papa Paskali I kumtia taji la kifalme Lotari I, mwana wa Pius, mahusiano yalizidi kuharibika.

Papa Paskali I alipokea wamonaki wengi kutoka Dola la Roma Mashariki waliokimbia dhuluma ya serikali kuhusu picha takatifu[8], akawapa kazi ya kupamba makanisa aliyoyajenga au kuyakarabati[6][9] pamoja na kuwatetea kwa maandishi yake [10].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu[11][5], hasa tarehe 11 Februari[12][13] au 14 Mei[14][15].

Remove ads

Tazama pia

Maandishi

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads