From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane mwana wa Zebedayo alikuwa mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu, ambaye alipendwa na mwalimu wao kuliko wenzake wote.
Mitume wa Yesu |
---|
|
Mapokeo ya Kikristo yanamuona kuwa mwandishi wa Injili ya Yohane, wa barua tatu (Waraka wa kwanza wa Yohane, Waraka wa pili wa Yohane, Waraka wa tatu wa Yohane) na wa Kitabu cha Ufunuo.
Alizaliwa na Salome baada ya Yakobo Mkubwa mwanzoni mwa karne ya 1 B.K. akafa mkongwe mwishoni mwa karne hiyo huko Efeso (katika Uturuki wa leo).
Kabla ya kumfuata Yesu Kristo alikuwa mvuvi na mfuasi wa Yohane Mbatizaji.
Ndiye shahidi mkuu wa miaka mitatu hivi ya utume wa Yesu, akiwa wa kwanza kumfuata (pamoja na Mtume Andrea), mshiriki wa matukio ya pekee ya mwalimu wake (kama alipogeuka sura mlimani), mtume pekee aliyesimama chini ya msalaba, wa kwanza kusadiki ufufuko wa Yesu hata kabla hajamuona.
Kutokana na udhati wa teolojia yake alifananishwa na tai.
Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu karibu yote ya Ukristo kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Desemba[1].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.