Malaysia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Malaysia, rasmi kama Shirikisho la Malaysia, ni nchi katika Asia ya Kusini-mashariki, inayojumuisha Rasi ya Malay na sehemu ya kaskazini ya kisiwa cha Borneo, pamoja na visiwa vichache vidogo.Inapakana na Uthai kaskazini, Singapore kusini, Brunei na Indonesia mashariki. Mnamo 2024 Malaysia ina idadi ya watu takriban milioni 34, ikiwa ya 44 duniani. Jiji lake kubwa zaidi ni Kuala Lumpur, ambalo pia ni mji mkuu. Malaysia inajulikana kwa utofauti wake wa kitamaduni, rasilimali asili tajiri, na maendeleo ya haraka ya uchumi, ikifanya kuwa nchi muhimu katika Asia ya Kusini-mashariki. Kisiasa Malaysia ni shirikisho la majimbo 13 na maeneo ya shirikisho 3.

Remove ads
Historia
Nchi ilianzishwa mwaka 1963 wakati Shirikisho la Kimalay (kwa Kimalay: Persekutuan Tanah Melayu) liliungana na Singapur, Sabah na Sarawak ambazo awali zilikuwa chini ya Uingereza.
Hata hivyo Singapur iliondoka mwaka 1965 ikawa nchi ya pekee.
Utawala
Majimbo ya Shirikisho
Malaysia ni Shirikisho la Kifalme. Tisa kati ya majimbo yake 13 ni sultani chini ya utaratibu wa kifalme na manne hufuata muundo wa jamhuri.
Majimbo ya shirikisho ni kama yafuatavyoː
Sultani tisa zinazoongozwa na Sultani pamoja na waziri mkuu anayechaguliwa na bunge la jimbo:
- Johor,
- Kedah,
- Kelantan,
- Negeri Sembilan,
- Pahang,
- Perak,
- Perlis,
- Selangor
- Terengganu
Majimbo manne chini ya gavana anayeteuliwa na serikali kuu na waziri mkuu anayechaguliwa na bunge la jimbo:
Maeneo matatu ya shirikisho:
- Putrajaya
- Kuala Lumpur
- Labuan.
Remove ads
Demografia
Wakazi ni mchanganyiko mkubwa, lakini Wamalay (50.1%) na wakazi asili wengine walio Waislamu wanapewa na katiba ya nchi nafasi ya pekee. Wachina ni 22.6%. Wahindi ni 7.3%
Lugha rasmi ni Kimalay, lakini zinatumika pia lugha nyingine 136.
Dini rasmi ni Uislamu unaofuatwa na 61.3% za wakazi (wengi wakiwa Wasuni), wakati 19.8% ni Wabuddha, 9.2% ni Wakristo, 6.3% ni Wahindu, 1.3% ni wafuasi wa dini za Kichina (Ukonfusio na Utao).
Tazama pia
Viungo vya Nje
- (Kiingereza) Tovuti rasmi
- (Kiingereza) Ramani ya Malaysia
- Malaysia at Encyclopædia Britannica
- Malaysia entry at The World Factbook
- Malaysia Ilihifadhiwa 23 Januari 2009 kwenye Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Malaysia katika Open Directory Project
- Malaysia profile from the BBC News
- Wikimedia Atlas of Malaysia
- Key Development Forecasts for Malaysia from International Futures
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Malaysia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads