Abia (jimbo)

jimbo nchini Nigeria From Wikipedia, the free encyclopedia

Abia (jimbo)
Remove ads

Abia ni jimbo la kujitawala la Nigeria lenye wakazi milioni 4.2 (2005) na eneo la km² 5,834. Mji mkuu ni Umuahia na mji mkubwa Aba wenye wakazi 900,000.

Thumb
Ramani.
Thumb
Abia.

Eneo

Abia imepakana na majimbo ya Enugu, Ebonyi, Cross River, Akwa Ibom, Rivers, Imo na Anambra. Haina pwani.

Mito muhimu ni mto Imo na mto Aba inayoelekea kwenye delta ya mto Niger.

Kusini mwa jimbo ni tambarare ya chini yenye mvua nyingi. Maeneo ya kaskazini ni ya juu kidogo.

Uchumi

Uchumi umetegemea hasa kilimo. Nafaka, minazi, mahindi, mpunga, muhogo, matunda na mboga hulimwa.

Kuna pia madini yanayochimbwa: ni hasa zinki, mchanga, chokaa pia kiasi cha mafuta ya petroli. Abia hukorogwa bia na kuna viwanda vya nguo na kioo.

Wakazi

Watu wa Abia ni hasa wa kabila la Igbo.

Makala hii kuhusu maeneo ya Nigeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Abia (jimbo) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads