Waalkantara
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Waalkantara (jina rasmi: Ndugu Wadogo Pekupeku) walikuwa tawi la utawa wa Fransisko wa Asizi lililotokana na juhudi za kuleta urekebisho za Petro wa Alkantara (1499 - 1562). Juhudi hizo nchini Hispania zilifuata zile za namna hiyo za Yohane wa Puebla (1453 - 1495) na Yohane wa Guadalupe (karne ya 15 - 1506), ambaye wafuasi wake waliitwa Wakonventuali Wareformati wakajulikana zaidi kama Waguadalupe.

Yeye alihamia kanda ya Wapaskwali, walioitwa hivyo kwa heshima ya Yohane Pascual (karne ya 15 - 1553), akaistawisha kwa mafanikio makubwa[1]. Ndiyo sababu wafuasi wakaja kuitwa kwa kawaida Waalkantara [2].
Ni kwamba baadhi ya Waguadalupe, baada ya kuunganishwa na Waoservanti (1517) walimkimbilia Mkuu wa Wakonventuali ili kukwepa vizuio vya OFM, na Petro wa Alkantara akafanywa Mkurugenzi wao (1557)[3]. Alipofariki dunia, Papa Pius IV (1560-1565) akawahamisha Waalkantara chini ya Waoservanti lakini bila ya kufuta kanda zao, katiba yao wala mavazi yao maalumu [2]. Papa Gregori XIII (1572-1585) akamkataza Mkuu wa OFM asiingilie masuala yao ya ndani (1578), na Papa Urban VIII (1623-1644) akawaruhusu wasifuate tena katiba ya shirika lote (1642).
Jinsi sisitizo la sala na toba linavyozaa matunda imethibitishwa na umisionari wao (Amerika na Asia Mashariki) na hasa na watakatifu 9 wa urekebisho huo, wakiwa ni pamoja na Paskali Baylon (+1592), mwenye ibada ya pekee kwa Ekaristi, Petro Batista, Martino wa Kupaa na Fransisko Blanco, mapadri, halafu Fransisko wa mt. Mikaeli, Gonzalo Garcia na Filipo wa Yesu, mabradha, ambao wote walifia dini Japani (+1597), hatimaye nchini Italia Yohane Yosefu wa Msalaba (+1734), mpenda ufukara mkuu, na Egidi Maria wa Mt. Yosefu (+ 1812), ombaomba mnyenyekevu sana [4]. Pia walipatikana wenye heri 22.
Mwaka 1895 Papa Leo XIII aliupendekezea mkutano mkuu muungano wa matawi OFM uwe ajenda kuu, na Kardinali akaeleza namna ya kuyaunganisha. Waoservanti wote wakakubali, Warekoleti vilevile kwa sharti la kutunza ufukara kwa uangalifu, kumbe Wariformati na Pekupeku walio wengi wakakataa; jumla ya kura ikawa 77 ndiyo na 31 hapana. Basi kamati ikaandaa katiba mpya iliyothibitishwa mwaka 1897, halafu Papa Leo XIII akatangaza rasmi muungano kamili wa matawi yote chini ya Mtumishi mkuu tu, ambao uonekane wazi hata kwa nje (kanzu ya mtindo mmoja badala ya ainaaina na rangi ya kahawia badala ya zile tofauti za awali: nyeusi, ya kijivu, ya zambarau na ya baharia). Akaagiza kanda zisizokubali wasiweze kupokea wanovisi tena, na watawa binafsi wasiokubali wapangiwe nyumba maalumu ambapo wakae wao tu, bila ya kuchanganyikana na walioungana[4]. Hata hivyo muungano haukufanikiwa vizuri; Wahispania walikubali katiba lakini wakaendelea kujiongoza kitaifa hadi 1932; hasa majaribio ya kuunganisha katika kanda moja Wafransiskani wa matawi mbalimbali yalisababisha ushindani mwingi hadi juzijuzi.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
